Ijumaa, 30 Desemba 2016

Taifa Jangombe imefanikiwa kupata ushindi kwenye uzinduzi wa Mapinduzi Cup Seif Hassan ‘Banda’ amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga bao kwenye michuano ya Mapinduzi Cup msimu huu baada ya kuifungia timu yake bao pekee la ushindi wakati wa mchezo wa ufunguzi kati ya Taifa Jang’ombe dhidi ya Jang’ombe Boys mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Amaan, Zanzibar. Banda aliifungia bao Taifa Jang’ombe dakika ya 83 na kuifanya timu yake iongoze Kundi A kwa kuwa na pointi moja mkononi baada ya kucheza mchezo mmoja. Mechi hiyo ilikuwa na upinzani mkubwa kutokana na timu zote kutoka mtaa mmoja hivyo kukamiana na kutambiana nje na ndani ya uwanja kulisababisha mechi hiyo kuwa ya upinzani mkali. Baada ya mchezo huo, Kesho (Jumamosi) hakutakuwa na mechi, Jumapili ratiba ya Mapinduzi itaendelea lakini mechi inayosubiriwa kwa hamu ni kati ya Taifa Jangombe dhidi ya Simba SC ambayo inatarajiwa kuwasili Zanzibar kesho (Jumapili).

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni