Jumanne, 20 Desemba 2016

JAMES AKUBALI KUACHANA NA MADRID, AITA CHELSEA, ZIDANE AMUWASHIA TAA ZA KIJANI Mshambuliaji wa Real Madrid, James Rodriguez sasa anaonekana amechoka kusbiri nafasi ya kucheza katika kikosi cha Real Madrid. Anataka kuondoka na kujiunga na vinara wa Premier League, Chelsea. Kocha Zinedine Zidane amemuambia anaweza kwenda kujaribu maisha kwingine. Pamoja na ruhusa hiyo, awali ilionekana lama James amekuwa havutiwi kuondoka Valdebebas na kujiunga na timu nyingine. Tokea amejiunga na Madrid akitokea Monaco, James amekosa mamba ya kudumu katika kikosi cha Zidane.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni