Ijumaa, 23 Desemba 2016

Jose Mourinho: Pesa za China zinavutia. Kwa sasa hivi ukizungumzia pesa na soka basi hautaacha kuitaja ligi ya China ambayo inatumia pesa nyingi sana ili kuwaleta wachezaji maarufu kwenye ligi yao. Leo tumeshuhudia jinsi Oscar alivyo break internet jinsi alivyoweka rakodi ya kuwa mchezaji anayelipwa pesa nyingi duniani baada ya kutamburishwa rasmi kama mchezaji wa Shanghai SIGP. Kwa upande wa kocha Jose Mourinho ambaye anaingoza club ya Manchester united ameulizwa kuhusu kujiunga na ligi hiyo na Sky Sport a haya ni majibu yake, “Pesa za China zinavutia kwa kila mtu. Lakini napenda sana soka langu kwa level hii. Nina miaka 53 mimi bado ni mdogo sana kwenye nafasi yangu. Mimi ni mdogo kwenda sehemu kama China, nataka kuendelea kushinda mataji kwenye ligi ngumu. KWa hiyo nipo kwenye sehemu nzuri”. Pia aliongezewa swali la kupewa ofa ya mkataba mpya wa miaka mingi na uongozi wa Manchester na je washauri wake wakimshauri asi sign kwa muda mrefu itakuaje,“Mimi napenda kuwa hapa na vingozi wa Manchester hawajanipa ofa yoyote mpya zaidi ya mkataba zaidi ya huu nilionao sasa hivi. Kuhusu kuongeza mkataba hapa hata washauri wangu wakinikataza mimi nita sign kwasababu hapa ndipo ninapotaka kuwa”.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni