Alhamisi, 22 Desemba 2016

Tanzania yapanda viwango FIFA Shirikisho la Soka Duniani, FIFA limetangaza viwango vipya vya ubora vya mchezo huo kwa mwezi huu ikiwa ni orodha ya mwisho kabisa kwa mwaka huu. Tanzania imepanda kwa nafasi 4 na kuwa ya 156 katika viwango hivyo katika mwezi ambao haukuwa na mabadiliko makubwa kutokana na uchache wa mechi za kimataifa. Hakuna mabadiliko katika nafasi kumi za juu Duniani huku Argentina ikiendelea kuwa kinara ikifuatiwa na Brazil na Ujerumani na Chile. Kwa upande wa Afrika, Senegal imesalia kileleni katika nafasi ya 33 duniani ikifuatiwa na Ivory Coast na Tunisia. Uganda imeendelea kuwa kinara ukanda wa Afrika Mashariki kwa kukamata nafasi ya 72 duniani ikifuatiwa na Kenya katika nafasi ya 89 na Rwanda katika nafasi ya 92.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni