Jumanne, 20 Desemba 2016

HAONDIKI! TOURE ASEMA ANATAKA KUBAKI CITY AISAIDIE KUWA KUBWA KULIKO MAN UNITED Awali ilionekana kama angeondoka lakini Yaya Toure amesema anataka kubaki Manchester City. Toure amesema angependa kuwa msaada wakati Man City inapiga hatua na kuwa kubwa kuliko Man United. Raia huyo wa Ivory Coast amekuwa hana uhusiano mzuri na Kocha wake, Pep Guardiola ambaye alipotua tu Man City, alianza kumuandama ikiwa ni pamoja na kumtoa kikosini. Lakini taarifa zinaeleza Toure amekuwa akifanya juhudikumaliza tofauti yake na Pep ambaye pia alikuwa kocha wake zamani Barcelona. Toure analipwa mshahara mkubwa wa pauni 230,000 kwa wiki.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni