Jumatano, 28 Desemba 2016

BREAKING NEWS: AZAM FC IMEWATIMUA MAKOCHA WAKE WOTE RAIA WA HISPANIA Azam FC imemtimua Kocha wake Mkuu, Zeben Hernandez. Zeben na makocha wengine raia wa Hispania, wametimuliwa kazi leo baada ya Azam FC kwenda mwendo wa kusuasua. Azam FC iko katika nafasi ya nne ikiwa na pointi 27 baada ya kucheza mechi 17. Katika mechi 17 za Ligi Kuu Bara, Azam FC imechinda mechi saba, imepoteza nne na sare sita, hali ambayo wazi inaonekana kutoufurahisha uongozi wa Azam FC hata kidogo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni