pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumamosi, 24 Desemba 2016
LIVE KUTOKA UWANJA WA UHURU: SIMBA 1 VS 0 JKT (MAPUMZIKO) MAPUMZIKO -Wachezaji wa JKT wanaonekana kumzonga mwamuzi hapa wakilalamika kwamba kipa wao alikuwa chini -Kipa bado yuko chini anatibiwa na mwamuzi akiwa anasubiri, anainuka hapa GOOOOOOOOO DK 45+2, Muzamiru anaifungia Simba bao akiunganisha krosi ya Athanas, wakati huo kila Seif alikuwa chini baada ya kugongwa, hakuinuka DAKIKA 3 ZA NYONGEZA Dk 44, Kipa Hamisi Seif wa JKT, mwenyewe anakwenda hadi chini na kukaa. Sasa anatibiwa Dk 43, Simba wamefanya shambulizi mfululizo kwa dakika moja nzima lakini JKT wamekuwa makini kuokoa, kipa wao wao Hamisi Seif anakuwa makini zaidi Dk 38, Simba wanahamia kwenye lango la JKT, wanafanya mashambulizi matatu mfululizo lakini JKT wanaonekana wako makini kuokoa DK 36, JKT wanafanya shambulizi jingine kali lakini shuti la Juma halikulenga lango Dk 33, krosi safi inamkuta Kichuya, anajaribu shuti baiskeli lakini mpira unatoka nje Dk 32, JKT wanapata kona baada aya kufanya shambulizi la kushitukiza, inachongwa na Mussa Juma, mpira unamkuta Mkude anaokoa Dk 29, kipa wa JKT yuko chini baada ya kuumizwa, anapatiwa matibabu huku Simba wakisubiri kupiga kona Dk 27, Simba wanapata kona ni baada ya kuendelea kupeleka presha kubwa kwenye lango la JKT Dk 23, kipa Hamisi Seif anaokoa kwa ukaribu shuti la Muzamiru baada ya krosi safi ya Pastory Dk 22 sasa, JKT wanabaki nyuma kwa wingi, wakiacha mtu mmoja tu na wanafanya mashambulizi ya kushitukiza Dk 21, JKT wanafanya kazi ya ziada kuwazuia Simba baada ya kugongeana vizuri wakiingia kwenye lango lao KADI Dk 20 Kotei naye analambwa kadi ya njano kwa kufanya madhambi KADI Dk 19 Edward Joseph analambwa kadi ya njano kwa kubaki na mpira baada ya filimbi Dk 17, Athanas anaingia vizuri hapa na kupiga shuti, beki wa Yanga anazuia na kipa anadaka vizuri KADI Dk 15, Salim Aziz Gilla analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Athanas Dk 11, Joseph wa JKT anaonyesha uwezo mkubwa kwa kuachia shuti kali lakini kipa Agyei anaonyesha umahiri kwa kuokoa na kuwa kona, isiyo na matunda Dk 7, Pastory anajaribu vizuri hapa akiunganisha pasi ya Kichuya lakini shuti lake halikulenga lango Dk 5 sasa, Simba wanaendelea kupanga mashambulizi lakini bado mpira zaidi unachezwa katikati ya uwanja Dk 2, Banda anapiga vizuri hapa mpira wa adhabu, lakini kipa JKT anaonyesha umakini mkubwa Dk 1, Pastory alikuwa anaondoka lakini anaangusha na kuwa faulo Dk 1, mechi inaanza kwa kasi ikionyesha kila timu imepania kupata bao la mapema, JKT ndiyo wanaanza mpira na Simba wanafanya madhambi
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni