pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumamosi, 24 Desemba 2016
BAADA YA CHEKA KUSEMA HAPANDI ULINGONI LEO, PROMOTA ASEMA ATAMFIKISHA MAHAKAMANI, ATUPIA PICHA AKIHESABU FEDHA ALIZOLIPWA Baada ya bondia Francis Cheka kutangaza hatapanda katika pambano lake dhidi ya Dulla Mbabe leo, promota wa pambano hilo Kaike Siraju ameibuka na kusema atamfikisha mahahamani. Siraji amesema atamfikisha Cheka mahakamani kama atashindwa kupanda ulingoni kwa kuwa ameishachukua fedha ya kutanguliziwa.. Pambano hilo linalofanyika jijini Dar es Salaam, linasubiriwa kwa hamu kuu na mashabiki wa ngumi, lakini Cheka ametupia kwenye mtandao wa Facebook akisema, hajalipwa. Lakini Kaike naye ametupia picha mtandaoni akionyesha Cheka ameishalipwa na anaonekana akihesabu fedha na baadaye anasaini mkataba. Kumekuwa na taarifa kwamba kuna malumbano na kuwekeana fitna kati ya mapromota Jay Msangi aliyempeleka India na Kaike Siraju ambaye ameandaa pambano la leo. Cheka alikwenda kupigana na India na kutwangwa kwa TKO katika raundi ya tatu huku akiwa anasubiriwa na pambano jingine gumu la Dulla Mbabe ndani ya siku nane tu.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni