pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Ijumaa, 23 Desemba 2016
LIVE KUTOKA UWANJA WA UHURU: AFRICAN LYON 0 VS 0 YANGA DAKIKA 3 ZA NYONGEZA Dk 45, kona inachongwa safi, Bossou anaruka na kumgonga kipa wa Lyon, yuko chini hapa anatibiwa na wachezaji wa Lyon wanamvaa Bossou Dk 44, MSuva anapiga mpira unamgusa mlinzi wa Lyon, kona. Inachongwa, Lyon wanaokoa tena, kona Dk 44, krosi nzuri ya Kaseke, mpira unamfikia Kamusoko lakini Lyon wanaokoa hapa Dk 39, krosi nzuri ya Niyonzima, MSuva anapiga kichwa safi hapa, kipa anajitahidi kuokoa na mwamuzi anasema ni offside Dk 37 sasa, ndani ya dakika nne, Lyon wamefika kwenye lango la Yanga mara tatu, inaonekana wanazidi kuongeza mashambulizi taratibu Dk 31, Mguhi yuko chini pale, anaonekana atakuwa ameumia baada ya kupiga kichwa ule mpira Dk 30, Lyon wanafanya shambulizi zuri hapa, Mguhi anapiga kichwa safi lakini mpira wake haukulenga lango DK 29 sasa, bado mpira unachezwa zaidi katikato ya uwanja na mashambulizi dhaifu ndani ya 18 kwa kila upande KADI Dk 28, Bossou naye analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Abdallah Mguhi KADI Dk 24, Manzi analambwa kadi ya njano kwa kumgonga Niyonzima Dk 22, Yanga wanaingia vizuri, Juma anapiga krosi safi, wanaokoa Lyon na kuwa kona. Inachongwa lakini haina madhara Dk 21 sasa, inaonekana Yanga imeshindwa kuifungia difensi ya Lyon ambayo imejaza zaidi ya walinzi wanne na viungo watatu nyuma ya mpira Dk 19, mpira wa adhabu wa Juma Abdul, unamkuta Bossou anapiga kichwa kisicholenga lango, goal kick Dk 17, Lyon wanaonekana kuanza kufanya mashambulizi madogomadogo ya kushitukiza Dk 16, Dida anafanya kazi nzuri ya kuruka na kuudaka mpira wa Abdallah Mguhi Dk 11, shambulizi la kwanza la Lyon langoni mwa Yanga, krosi nzuri kabisa lakini Yanga wanaokoa vizuri kabisa Dk 8 sasa, bado mpira unaendelea kuchezwa zaidi katikati ya uwanja Dk 5, Hassan Isihaka yuko chini pale anatibiwa baada ya kugngana na Tambwe Dk 3, Niyonzima anatoa pasi nzuri kwa Juma Abdul, anapiga krosi nzuri lakini Tambwe anapiga kichwa kinachopaa mpira unapaa juuu Dk 1, mechi imeanza na Yanga ndiyo wanaonekana kupania kupata bao la mapema, lakini Lyon wameanza wengi zaidi wakiwa nyuma.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni