pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumanne, 20 Desemba 2016
AKILIMALI KWA MARA YA KWANZA AFUNGUKA KUHUSIANA NA SUALA LA WACHEZAJI YANGA KUGOMA Katibu wa Baraza la Wazee wa Yanga, Ibrahim Akilimali amewataka wachezaji waachane na mgomo na warejee kazini. Pamoja na kuwaomba wachezaji warejee kazini, ameutaka uongozi kukaa na kuzungumza na wachezaji wake. Akilmali alikuwa akizungumzia suala la wachezaji kugoma na kusababisha kutofanya mazoezi kwa siku mbili, juzi na jana kwa madai ya kutolipwa mshahara wa mwezi uliopita. “Wachezaji lazima wajue mambo hayo hutokea, hivyo wanapaswa kurejea kazini na kuachana na mambo ya migomo. Wafanye kazi huku wakijua suala lao linaweza kushughulikiwa. “Lakini uongozi nao ulishughulikie suala hili kwa kukutana na wachezaji wake na kulijadili suala hilo ili walimalize. Sisi kama viongozi tuko tayari kuwaunga mkono,” alisema Akilimali
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni