pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumanne, 20 Desemba 2016
WACHEZAJI, UONGOZI YANGA WAKUBALIANA, WACHEZAJI KUREJEA MAZOEZINI LEO ASUBUHI Uongozi wa Yanga na wachezaji wamefikia makubaliano kwa pamoja kwamba kazi ziendelee kama kawaida. Kwa maana hiyo wachezaji wataendelea na mazoezi, leo asubuhi. Uongozi utalishughulikia suala la mishahara na hadi leo jioni au kesho Alhamisi malipo ya wachezaji wa Yanga yawe yamekamilika. Maana yake, kwa makubaliano hayo, suala la mgomo wa siku mbili ambao ulianza kuripotiwa na blog hii jana, utakuwa umefikia tamati. Wachezaji wa Yanga waligoma kufanya mazoezi juzi, halafu jana wakitaka kulipwa fedha zao za mshahara wa Novemba. Pamoja na uongozi wa Yanga kupitia Katibu wake Mkuu, Baraka Deusdedit kupambana kuhakikisha wanalikanusha jambo hilo, mwisho ilishindikana. Lakini wachezaji wa Yanga, kesho wanatarajia kurejea mazoezini na kuendelea na maandalizi ya mechi dhidi ya African Lyon ambayo itapigwa Ijumaa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni