Jumatano, 21 Desemba 2016

SERIKALI YACHARUKA, YAWASTOPISHA WACHEZAJI YANGA, SIMBA, AZAM WASICHEZE BILA VIBALI ZULU, AMETUA YANGA AKITOKEA ZESCO YA ZAMBIA. AWALI ILIELEZA AMEPATA KIBALI, LAKINI HADI JANA HAKUWA AMEPATA NA YANGA WALIKUWA WAKIHAHA LEO KUPATA KIBALI. LAKINI SIMBA PIA HADI JANA HAWAKUWA WAMEPATA VIBALI VYA BAADHI YA WACHEZAJI WAO, NAO WALIKUWA WAKIHAHA LEO KAMA ILIVYOKUWA KWA AZAM FC. INAWEZEKANA WATAKUWA WALIPATA MCHANA WA LEO. Serikali imezicharukia Simba, Yanga, Azam FC na timu zote zinazoshiriki Ligi Kuu Bara ambazo wachezaji wao hawajapata vibali vya kufanya kazi nchini. Ofisa Uhamiaji wa jiji la Dar es Salaam, John Msumule amesema mchezaji yoyote ambaye atakuwa hajakamilisha suala la kibali cha kazi asithubutu kucheza wala kukaa kwenye benchi. “Hili ni agizo, kama mchezaji hana kibali cha kazi asifanye kazi na wala hakutakuwa na utani. Wote wanajua taratibu ni zipi, basi zifuatwe,” alisema. Leo mchana, Yanga na Simba walikuwa wakihaha katika ofisi za Mambo ya Ndani jijini Dar es Salaam kuhakikisha wanapata vibali hivyo. Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit na Katibu Mkuu wa Simba, Patrick Kahemele walionekana kwenye ofisi hizo. Lakini baadaye, Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba naye alifuatia ikionekana kila upande ulikuwa ukihaha kukamilisha taratibu hizo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni