pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Ijumaa, 23 Desemba 2016
LIVE KUTOKA UWANJA WA UHURU: AFRICAN LYON 1 VS 1 YANGA (FULL TIME) MPIRA UMEKWISHAAAAAAA KADI Kipa Rostand Youthe analambwa kadi ya njano kwa kupoteza muda kwa makusudi kabisa -Kipa wa Lyon anaendelea kuutumia muda huu kwa kujilaza. Anaonekana hajaumia lakini analenga kupoza presha ya mashambulizi ya Yanga DAKIKA 3 ZA NYONGEZA Dk 90, Juma Abdul anaingia krosi safi, Hassan Isihaka anawahi na kuokoa Dk 87, Yanga wanafanya shambulizi jingine, Tambwe anashindwa kulenga lango. Lyon wanalazimika kuwa makini kwa kuwa mara kadhaa wanamsahau Tamgwe SUB Dk 82, Cosmas Lewis anaingia kuchukua nafasi ya Thomas Maurice kwa upande wa Lyon KADI Dk 81, Omar Abdallah analambwa kadi ya njano kwa kupoteza muda wakati akitoka SUB Dk 80, Peter Mwalyanzi anaingia upande wa Lyon kuchukua nafasi ya Omar Abdallah Dk 79, krosi safi ya MWashiuya, krosi inaunganishwa na MSuva lakini hakuna kitu Dk 78 sasa, Yanga wanaonekana kushambulia mfululizo huku wakigongeana pasi nyingi zaidi huku Lyon wakionekana kupoteza ile hali ya kujiamini hasa katika ulinzi SUB DK 75 Geofrey Mwashiuya anaingia kuchukua nafasi ya Mwinyi Haji GOOOOOOO Dk 74, Tambwe baada ya kukosea zaidi ya mara tatu, anaisawazishia Yanga bao safi kabisa kwa kuunganisha krosi kwa kichwa Dk 69, krosi safi, Tambwe amebaki na kipa anaruka na kupiga krosi, juu. Hata hivyo mwamuzi anasema ni offside SUB Dk 65, Kaseke anakwenda benchi upande wa Yanga na nafasi yake anachukua Emmanuel Joseph ambaye amejiunga na Yanga akitokea JKU na hii ni mechi yake ya kwanza Dk 62, Yanga wanapata kona nyingine, inachongwa akini mwamuzi anasema hapa, kulikuwa na mpira mwingine ndani ya uwanja Dk 61, Yanga wanapata kona ya pili kipindi hiki na ya saba katika mchezo huu, inachongwa na Msuva, Tambwe anajitwika tena, lakini hajalenga Dk 61, krosi ya Juma Abdul, Tambwe anajitwika lakini ni mpira rahisi kwa kipa huyu Mcameroon GOOOOOOOOO Dk 59, Venance Ludovick aliyeingia kipindi cha pili anaifungia Lyon bao safi kabisa akiunganisha krosi maridadi kabisa SUB Dk 58, Yanga wanamtoa Kamusoko na nafasi yake inachukuliwa na Obrey Chirwa raia wa Zambia Dk 55, Tambwe katikati ya mabeki anaunawa mpira wakati Yanga ikishambulia. Kiasi fulani Yanga wanaongeza kasi ya mashambulizi Dk 53, krosi safi ya MWinyi Haji, MSuva anajituma na kujitwika kichwa hapa, goal kick Dk 50, Lyon wanapata mpira eneo si mbali na eneo la Yanga, anachonga Miraji Adam lakini anapiga buuuu Dk 47, Juma Abdul tena anaachia shuti kali, linapita juu ya lango la Lyon Dk 46, krosi safi ya Juma Abdul kwenda kwa Kamusoko lakini Lyon wanaokoa na kuwa kona DK 46, Yanga wanakuwa wa kwanza kufika kwenye lango la Lyon, lakini ni goal kick SUB Dk 46, Venance Ludovick anaingia kuchukua nafasi ya Awadhi Juma ambaye inaonekana atakuwa aliumia mwishoni mwa kipindi cha kwanza KADI Makapu anapambwa kadi ya njano kwa kumfanyia madhambi Awadhi Juma -Sasa ni dakika ya 45+5, Niyonzima anajaribu shuti kali kabisa, lakini mpira unatoka juu. Yanga wanaonekana kuonana vizuri lakini wanashindwa kuipita ngome ya Lyon MAPUMZIKO DAKIKA 3 ZA NYONGEZA Dk 45, kona inachongwa safi, Bossou anaruka na kumgonga kipa wa Lyon, yuko chini hapa anatibiwa na wachezaji wa Lyon wanamvaa Bossou Dk 44, MSuva anapiga mpira unamgusa mlinzi wa Lyon, kona. Inachongwa, Lyon wanaokoa tena, kona Dk 44, krosi nzuri ya Kaseke, mpira unamfikia Kamusoko lakini Lyon wanaokoa hapa Dk 39, krosi nzuri ya Niyonzima, MSuva anapiga kichwa safi hapa, kipa anajitahidi kuokoa na mwamuzi anasema ni offside Dk 37 sasa, ndani ya dakika nne, Lyon wamefika kwenye lango la Yanga mara tatu, inaonekana wanazidi kuongeza mashambulizi taratibu Dk 31, Mguhi yuko chini pale, anaonekana atakuwa ameumia baada ya kupiga kichwa ule mpira Dk 30, Lyon wanafanya shambulizi zuri hapa, Mguhi anapiga kichwa safi lakini mpira wake haukulenga lango DK 29 sasa, bado mpira unachezwa zaidi katikato ya uwanja na mashambulizi dhaifu ndani ya 18 kwa kila upande KADI Dk 28, Bossou naye analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Abdallah Mguhi KADI Dk 24, Manzi analambwa kadi ya njano kwa kumgonga Niyonzima Dk 22, Yanga wanaingia vizuri, Juma anapiga krosi safi, wanaokoa Lyon na kuwa kona. Inachongwa lakini haina madhara Dk 21 sasa, inaonekana Yanga imeshindwa kuifungia difensi ya Lyon ambayo imejaza zaidi ya walinzi wanne na viungo watatu nyuma ya mpira Dk 19, mpira wa adhabu wa Juma Abdul, unamkuta Bossou anapiga kichwa kisicholenga lango, goal kick Dk 17, Lyon wanaonekana kuanza kufanya mashambulizi madogomadogo ya kushitukiza Dk 16, Dida anafanya kazi nzuri ya kuruka na kuudaka mpira wa Abdallah Mguhi Dk 11, shambulizi la kwanza la Lyon langoni mwa Yanga, krosi nzuri kabisa lakini Yanga wanaokoa vizuri kabisa Dk 8 sasa, bado mpira unaendelea kuchezwa zaidi katikati ya uwanja Dk 5, Hassan Isihaka yuko chini pale anatibiwa baada ya kugngana na Tambwe Dk 3, Niyonzima anatoa pasi nzuri kwa Juma Abdul, anapiga krosi nzuri lakini Tambwe anapiga kichwa kinachopaa mpira unapaa juuu Dk 1, mechi imeanza na Yanga ndiyo wanaonekana kupania kupata bao la mapema, lakini Lyon wameanza wengi zaidi wakiwa nyuma.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni