Jumapili, 25 Desemba 2016

HAJI MANARA AMWOMBEA MSAMAHA JERRY MURO KWA RAIS WA TFF AMRUHUSU KUENDELEA NA KAZI Katika hali isiyotarajiwa na wadau wengi wa soka nchini Msemaji wa Simba, Haji Manara amemwombea msamaha msemaji mwenzake na Mkuu wa Kitengo cha Mawasliano wa Yanga, Jerry Muro kwa Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Jamal Malinzi amruhusu kuendela na majukumu yake baada ya kufungiwa mwaka mmoja kujihusisha na soka. Manara amemwomba Malinzi kupitia akaunti yake ya Instagram kwa kuandika kuwa anafahamu kuwa Jerry Muro alifanya makosa lakini kwa muda ambao amekuwa kifungoni anaamini atakuwa amejifunza na atajirekebisha kwa kufanya kazi bila kuvunja mipaka ya kazi ambayo amewekewa. Amesema uwepo wa Jerry Muro katika soka unafanya kuwepo na utani wa jadi kwa Simba na Yanga ulio na nguvu tofauti na sasa ambapo ni wazi unaonekana kupoa kutokana na Muro kuwa kifungoni. Jerry Muro alifungiwa kujihusisha na soka kwa kipindi cha miezi 12 [mwaka mmoja] na kutakiwa kulipa faini ya milioni tatu na Kamati ya Maadili ya TFF Julai, 7 mwaka huu baada ya kukutwa na makosa ya kuipinga na kuishambulia TFF kwa kutumia vyombo vya habari.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni