pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumatano, 21 Desemba 2016
Aliyepona kwenye Ajali ya Chapecoense, Aahidi kurejea Uwanjani Beki wa klabu inayoshiriki ligi kuu nchini Brazil ya Chapecoense, Alan Ruschel amesema anamwachia mwenyezi Mungu uhai wake kwani ndiye pekee aliyemwokoa baada ya ile ajali ya ndege iliyotokea mwezi ulipotea. Ruschel aliketi jirani na siti za nyuma za ndege kabla ya mkurugenzi wa klabu hiyo Cadu Gaucho hajamwomba kusogea mbele zaidi wakati wanalekea kwenye fainali ya Copa Sudamericana. ‘Cadu Gaucho aliniomba nisogee mbele zaidi kuketi na kuwaacha wanahabari waketi pamoja nyuma,’ Ruschel alisema katika mahojiano yake kwa ajali waliyokutana nayo November 28. Alan Ruschel anaamini mabadiliko ya siti hayo ndo inawezekana ikawa sababu ya kuokoa maisha yao. Chapecoense walikumbwa na tukio baya la kupoteza maisha ya watu 71 waliofariki kwenye ajali ya ndege iliyotokea katika safari ya kuelekea Colombia. ‘Sikutaka kuhama lakini nilipomwona (Jackson) Follman akanambia niketi pembeni yake,’ aliongeza. ‘Mungu pekee ndiye anayeweza kufahamu ilikuwaje nikasalimika. Alinishika na kunipa nafasi ya pili ya kuishi.’ Ruschel, 27, alikuwa miongoni mwa watu 6 waliosalimika kwenye ajali ya ndege, iliyotokea kwenye milima ya Medellin. Golikipaer Follman, moja ya marafiki wakubwa wa Ruschelkwenye timu pia alisalimika kwenye ajali hiyo lakini ilibidi akatwe sehemu ya mguu wake. Alisafirishwa siku ya Jumamosi kutoka Sao Paulo kuelekea hospitali ya mji wa nyumbani wa klabu hiyo kusini mwa Brazil. ‘Sikumbuki lolote kuhusiana na ajali,’ alisema Ruschel alisema kwenye Arena Conda, uwanja wa nyumbani wa klabu hiyo huko Chapeco. Ruschel akiwapungia mashabiki walokuja kumwona wakati akitoka hospitali. Ruschel aliweza kusimama na kuelekea kwenye gari iliyokuwa nje ya hospitali aliyokuwa amelazwa. Beki wa pembeni huyo ni moja kati ya watu sita waliopona katika ndege hiyo iliyowapa mkosi wa maisha Chapecoense. Ruschel ameahidi kurejea Colombia na kuwahudumia madaktari wa Colombia na moja ya vyakula vizuri maarufu huku Kusini mwa Brazil. Pia ameahidi kuwatembelea familia ya nduguze wote waliopata ajali pamoja katika mji wao mdogo wa Chapeco. Ruschel (kulia) ameahidi kurejea uwanjani na kucheza tena soka na ndicho anachokiombea.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni