Jumamosi, 22 Oktoba 2016

MOJA KWA MOJA KUTOKA KAITABA: KAGERA SUGAR 2 VS 6 YANGA (FULL TIME)

MPIRA UMEKWISHAAAA DAKIKA 4 ZA NYONGEZA Dk 90 sasa, hakuna kipya, timu zinaonyesha kucheza zaidi katikati ya uwanja, Yanga wakiwa wameridhika huku Kagera wakionekana kuwa wamekata tamaa Dk 87, mpira wa kurusha wa Twite, Tambwe anagonga kichwa lakini Babu Ally anaokoa Dk 83 hadi 85 Yanga wanaendelea kucheza taratibu kwa kujiamini, lakini kama Kagera watazubaa, basi Yanga wanaweza kuongeza bao tena Dk 82, Danny Mrwanda ambaye amefunikwa na Yondani anageuka na kujaribu shuti lakini Dida anadaka vizuri Dk 79 hadi 81, Yanga wanaonekana kugongeana taratibu kwa mbwembwe kabisa,wakiupoza mchezo SUB Dk 78, Matheo Anthony anaingia kuchukua nafasi ya Kaseke SUB Dk 77, Amissi Tambwe anaingia upande wa Yanga kuchukua nafasi ya Obey Chirwa GOOOOOOO Dk 73, Ngoma anaifungia Yanga bao la sita, ameunganisha pasi ya MSuva baada ya kumzidi kasi Kavila Dk 72 Kagera wanapata kona na kushambulia, lakini inaonekana haina madhara na Yanga wanaokoa Dk 72 Kagera wanapata kona na kushambulia, lakini inaonekana haina madhara na Yanga wanaokoaGOOOOOO Dk 63, Chirwa anafunga bao la tano kwa Yanga, la pili kwake baada ya Ngoma kuuwahi mpira wa Juma Ramadhani aliyemrudishia kipa, lakini kipa Burhani akaokoa, mpira ukamkuta Chirwa ambaye amemlamba chenga na kupachika wavuni kwa mguu wa kushoto safi kabisa SUB Dk 60, anaingia Babu Ally kuchukua nafasi ya Godfrey Taita upande wa Kagera GOOOOOOO Dk 57, Kaseke anafunga bao kwa shuti kali kabisa akiunganisha pasi nzuri ya MSuva aliyegongeana vizuri na Niyonzima DK 56, beki Juma ramadhani anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira mzuri wa Niyonzima langoni mwake Dk 55, krosi nzuri ya Niyonzima, Msuva akiwa katika nafasi nzuri lakini anashindwa kulenga. Beki wa kati wa Kagera wanaonekana kama kuzubaa hivi SUB Dk 53, mkongwe Mbuyu Twite anaingia kuchukua nafasi ya Kessy ambaye ameumia DK 52, Kessy wa Yanga yuko chini akipatiwa matibabu, anatolewa nje Dk 52, Msuva anagongeana vizuri na Niyonzima ambaye anapiga shuti kali lakini hakulenga lango Dk 50, Msuva anaingia vizuri lakini badala ya krosi anajaribu kupiga shuti na mpira unatoka juuuu, goal kick GOOOOOOO Dk 48, Mbaraka Yusuf anaunganisha pasi fupi ya Mangoma na kuifungia Kagera Sugar bao la pili katika mchezo wa leo. Huyu ndiye aliyefunga bao la kwanza DK Dk 46 Ngoma anaingia vizuri lakini anageuka na kumpa pasi Niyonzima, lakini mpira wake unakuwa laini Dk 46, Mpira umeanza taratibu Kagera wakigonga pasi nyingi fupifupi MAPUMZIKO -Hatari kabisa kwenye lango la Kagera, Ngoma anapiga free header lakini unatoka nje sentimeta chache kabisa DAKIKA 2 ZA NYONGEZA Dk 45, mpira wa krosi kali ya Taifa, Dida anapangua na mabeki wa Yanga wanaondosha Dk 44 sasa, Yanga wanaonekana kuupoza mchezo na hawana haraka hata kidogo, wanagongeana taratibu kabisa hapa Dk 40, Yanga wanagongeana vizuri, Mwinyi anapiga krosi tamu kabisa lakini Juma ramadhani anawahi kuokoa na kuwa kona. Inachongwa tena, haina manufaaa Dk 38, Dida anafanya kazi ya ziada, anatoka nje ya 18 na kuokoa mpira miguuni mwa Ally Dk 37, Chirwa anaingia na kumdhibiti Juma Ramadhani, anatoa krosi safi kwa MSuva ambaye anapiga shuti, wanaokoa na kuwa kona. Inachongwa na Niyonzima lakini haina matunda Dk 35, Kagera wanafanya shambulizi, mpira mzuri na Mangoma anaachia shuti kali lakini Andrew Vicent anaweka kichwa na kuokoa KADI Dk 33, Kessy analambwa kadi ya njano kwa kumchezea rafu Taita DK 33, Ngoma na Msuva wanagongeana vizuri na krosi safi lakini Burhani anaokoa vizuri kabisa SUB Dk 31 Kagera wanamuingiza Ali Ramadhani kuchukua nafasi Japhet Makaray, Pia wanamtoa kipa Casillas na nafasi yake inachukuliwa na David Burhani Dk 30, Kagera wanaonekana kuwa wamepaniki sasa na wanakaba kibabe jambo ambalo linaweza kuwasumbua au kuwaponza kupata kadi Dk 28 sasa, Yanga wanaonekana wanaendelea kushambulia kwa kasi zaidi wakiwapa Yanga GOOOOOOOOOO Dk 26, Niyonzima anatoa krosi safi kabisa, Msuva anaachia shuti, Casillas anaokoa tena lakini Chirwa anauwahi na kuutupia wavuni, Yanga tatu KADI Dk 23, Selemani Mangoma wa Kagera analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Ngoma kwa makusudi GOOOOOO Dk 21, Niyonzima anageuka na kupiga shuti kali, Casillas anatema na Msuva anamalizia safi kabisa na kuiandikia Yanga bao la pili Dk 15, Ufudu wa Kagera anafanya kosa hapa, anaingia Chirwa hatari lakini Juma Ramadhani anawahi na kuondosha hatari hiyo DK 10 hadi 14, mpira zaidi unachezwa katikati ua uwanja na inaonekana timu zina nafasi ya kugongeana kwa kuwa uwanja ni safi kabisa Dk 9 Japhet Makalay anaingia vizuri baada ya kumtoka Kessy lakini krosi yake inaishia mikononi mwa Dida Dk 8, Msuva anaingia tena, krosi safi kabisa hatariiii lakini Casillas anatokea na hudaka vizuri kabisa Dk 6, Mangoma wa Kagera anaingia vizuri anaachia shuti kali kabisa lakini ni goal kick GOOOOOOOO Dk 5, Ngoma anaifungia Yanga bao la kusawazisha baada ya kufunga kwa kichwa akiunganisha krosi safi ya Simon Msuva GOOOOOOOOOO Dk 3, Mbaraka Yusuf anamtoka Yondani na kuachia mkwaju mkali unaomngonga Dante na kumpoteza maboya kipa Dida na unajaa wavuni Dk 1, Yanga wanaonekana kuanza kwa kasi kama wamepanga kupata bao la mapema ikiwezekana kumaliza kazi mchezo Kikosi cha Yanga SC leo dhidi ya Kagera Sugar 1. Deogratius Munishi 2. Hassani Kessy 3. Mwinyi Haji 4. Andrew Vicenti 5. Kelvin Yondani 6. Thabani Kamusoko 7. Saimoni Msuva 8. Haruna Niyonzima 9. Donald Ngoma 10. Obrey Chirwa 11. Deusi Kaseke Akiba - Beno Kakolanya - Oscar Joshua - Vicent Bossou - Mbuyu Twite - Geofrey Mwashuiya - Mateo Antony

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni