MAPUMZIKO
DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 45, JKT wanapata kona lakini haina mafanikio
Dk 44 Yanga wanapoteza wanapotez anafasi nyingine tena ya wazi hapa baada ya Msuva kuukosa mpira
KADI Dk 39 kadi ya kwanza katika mchezo huu inatoka, Kassim Kisengo wa JKT anazawadiwa baada ya kumuangusha Chirwa
Dk 37, nafasi nyingine kwa Yanga, Ngoma akiwa hatua tano na kipa, anapiga kichwa pembeni juuuuuu
Dk 35, krosi safi ya Kessy, Ngoma anabaki na kipa, anampa mikononi
Dk 34 Chirwa anawahadaa mabeki wa JKT, anapiga shuti safi kabisa, lakini kipa anapangua na mabeki wanaosha
Dk 30, yuko chini anatibiwa baada ya kugongwa na beki wa JKT wakati akiokoa mpira, anatoka nje na baadaye mwamuzi anamruhusu kuendelea na mchezo
Dk 29, Kessy anaachia shuti kali tena, lakini mpira unawababatiza mabeki wa JKT na kuokoa
Dk 27 sasa, Yanga ndiyo wanaonekana kumiliki zaidi mpira katikati ya uwanja lakini hakuna shambulizi kubwa hata moja
Dk 22, Atupele anampa Dilunga pasi safi kabisa lakini shuti lake, mpira unatoka sentimeta chache nje ya lango la JKT
Dk 19, Kessy anapiga mpira unakwenda moja kwa moja na kugonga mwamba wa juu, mabeki JKT wanaokoa
Dk 12, Kamusoko naye anashindwa kuukwamisha mpira wavuni akiwa amebaki na kipa. Yanga wanazichezea hizi nafasi na wanapaswa wawe makini sana
Dk 11, Yanga wanafanya shambulizi jingine, mpira unamfikia Chirwa akiwa na kipa peke yake, lakini anampa mikononi
Dk 10, Kaseke anawahadaa mabeki JKT na kutoa pasi safi kwa Msuva lakini anapiga shuti kuuubwaaaa
Dk 8, JKT wanachonga kona yao ya pili lakini mpira unaokolewa mbali kabisa na Yondani
Dk 7, Atupele Green anaingia vizuri na kuachia shuti kali, Yondani anazuia na kuwa kona, inapigwa inakuwa nje tena, kona
GOOOOOO DK 6 Chirwa anaifungia Yanga bao kwa shuti kali baada ya beki wa JKT kuanguka na kuuacha mpira nyuma, MSuva akauwahi na kumpa Chirwa ambaye amemaliza kazi
Dk 1, Yanga wanaanza kwa kufanya shambulizi na kupata kona ambayo inachongwa lakini JKT wanaokoa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni