Badaa ya ushindi wa Yanga wa mabao 10 katika mechi mbili, Kocha Joseph Omog amewataka wachezaji wake kuamka na kuhakikisha wanatumia nafasi wanazozipata. Simba imekuwa moja ya timu zinazopoteza nafasi nyingi za kufunga mabao katika mechi za Ligi Kuu Bara. Omog raia wa Cameroon ambaye mara kwa mara amekuwa akiwasisitiza wachezaji wake kuzitumia nafasi sasa ameamua kuweka msisitizo. “Kocha amesisitiza sana kuhusiana na kuzitumia nafasi, si unaona katika mechi mbili Yanga wana mabao 10 ya kufunga. Hivyo hili ni suala ambalo hata sisi tumekubali kulifanyia kazi,” alisema mmoja wa wachezaji wa Simba. Yanga imeifunga Kagera Sugar kwa maabo 6-2 halafu ikaivurumisha JKT Ruvu kwa mabao 4-0 katika mechi nyingine iliyopigwa jana. Simba inaongoza Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 29 baada ya kucheza mechi 11 huku Yanga ikiwa na pointi 24 baada ya mechi 11 pia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni