Jumanne, 25 Oktoba 2016

Griezmann mchezaji bora La Liga, Modric kiungo bora

Mshambualiji wa Atletico Madrid Antoine Griezmann ametajwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa La Liga kwenye hafla maalum iliyofanyika jijini Valencia jana. Griezmann ameshinda tuzo hiyo mbele ya wakali wa Barcelona Lionel Messi na Luis Suarez Mapema Alhamisi ya wiki iliyopita Cristiano Ronaldo alioongoza orodha ya wachezaji wanaowania tuzo ya Ballon d’Or akiwa na Messi, Suarez na Griezman, kufuatia mafanikio aliyopata kwenye klabu yake ya Real Madrid kwa kutwaa Champions League na kuwapa Ureno taji la Euro 2016, lakiniitu cha kushagaza hakuweka katika category kwenye tuzo za Liga, kitu ambacho kimewashangaza wengi sana. Luis Suarez amepata tuzo ya ufungaji bora pamoja na mshambuliaji bora sambamba na mshambuliaji mkongwe wa Athletic Bilbao Aritz Aduriz. Miamba mitatu ya La Liga Barcelona, Madrid na Atletico Madrid ndiyo iliyotawala kinyang’anyiro hicho na kujaza wachezaji wote 11 kwenye kikosi bora cha mwaka. Ubora wa safu ya ulinzi ya Atletico umetambuliwa vilivyo na watoa tuzo kufuatia Jan Oblak na Diego Godin kupata tuzo ya kipa na beki bora mtawalia, huku boasi wao Diego Simeone akipata tuzo yake ya tatu ya kocha bora ndani ya misimu minne akiwashinda kocha wa zamani wa Villarreal Marcelino na yule wa Celta Vigo Eduardo Berizzo huku Luis Enrique wa Barcelona ambaye amewahi kushinda tuzo mara mbili safari hii akikosa kabisa. “Ni jambo zuri sana kupata tuzo hii hapa, ambayo naamini nisingeipata bila ushirikiano mzuri kutoka kwa wachezaji wenzangu,” Godin alisema ambaye amempokonya tuzo hiyo beki wa Real Madrid Sergio Ramos aliyeshinda miaka minne mfululizo.” Nyota wa Real Madrid’s Luka Modric amepata tuzo ya kiungo bora wa La Liga, akiwazidi kiungo wa Barcelona Sergio Busquets na nahodha wa Villarreal Bruno Soriano ambao wameshika nafasi ya pili na tatu. Msimu wa 2013-14 Modric alishinda tuzo hiyo sambamba na nahodha wa Barca Andres Iniesta. Marco Asensio wa Real Madrid ameshinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi wa La Liga kufuatia kiwango bora msimu uliopita ambapo alikuwa akicheza kwa mkopo kunako klabu ya Espanyol.




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni