Jumatatu, 31 Oktoba 2016

Dondoo muhimu: EPL Weekend iliyopita

Na Athumani Adam Ligi kuu nchini England iliendelea siku ya Jumamosi na Jumapili kwa michezo tisa kufanyika kwenye viwanja mbali mbali. Baada ya kumalizika kwa mechi hizo za mzunguko wa kumi zipo rekodi mbali mbali ambazo zilitokana matokeo ya mechi hizo Makala hii inakusimulia takwimu muhimu ambazo ziliandikwa baada ya kumalizika kwa michezo hiyo ya wikiendi October 30 na 31. Namba 1 (Ander Herrera) Kwenye mchezo dhidi ya Burnley kiungo wa Man United, Herrera alipata kadi nyekundu kwenye dakika ya 68 ya mchezo. Kadi ambayo Herrera alioneshwa na mwamuzi Mark Clatternburg siku ya Jumamosi inakuwa kadi nyekundu ya kwanza ya Herrera kwenye ligi kuu nchini Uingereza. Mara ya mwisho kwa mchezaji wa Man Utd kuoneshwa kadi nyekundu kwenye uwanja wa Old Trafford ilikuwa mwaka 2014 ambapo nahodha Wayne Rooney alipata kadi kwenye mchezo dhidi ya Westbrom Namba 2 (Sunderland, Jack Wilshere) Klabu ya Sunderland ambayo ipo chini ya kocha David Moyes imekuwa timu ya kwanza kuwa na pointi chache zaidi ligi kuu England baada ya kucheza kucheza mechi kumi. Sunderland hadi sasa ina pointi mbili wikiendi walipoteza mchezo dhidi ya Arsenal kwa 1-4. Mara ya mwisho kushuhudia timu kuwa na pointi kama za Sunderland ilikuwa msimu wa 1995/96 kwa timu ya Man City. Pia Kiungo wa Arsenal aliye kwa mkopo kwenye klabu ya Bournemouth, Jack Wilshere alifanikiwa kucheza mechi ya pili kwa dakika zote tisini wikiendi hii. Bournemouth walipoteza dhidi ya Middlesbrough kwa mabao 2-0. Namba 3 (Vicent Janssen) Mshambuliaji wa Tottenham Hotspurs, Vicent Janssen aliifungia timu yake bao la kuongoza dakika ya 44 kwenye mchezo dhidi ya Leicester. Bao la Janssen linamfanya kuwa na mabao matatu kwenye klabu ya Spurs huku mabao yote akiwa amefunga kwa njia ya penati. Mara ya mwisho kwa Wlishere kucheza dakika tisini ilikuwa ni mwezi September 2014. Namba 4 (Chelsea) Kwenye mechi tano za karibuni, Klabu ya Chelsea inaonekana kuwa na safu bora ya ulinzi baada ya kupata Clean Sheet 4 (kucheza bila kuruhusu bao). Clean Sheet ya nne ya hivi karibuni ilikuwa siku ya Jumapili ambapo Chelsea ilipata ushindi wa 2-0 dhidi ya Southampton. Namba 6 (Zlatan Ibrahimovic) Ukame wa mabao umeendelea kwa mshambuliaji wa Man United Zlatan Ibrahimovic. Zimepita mechi sita tangu Ibrahimovic alipofunga mara ya mwisho kwenye mchezo dhidi ya mahasimu wao wa jiji la Manchester, Man City mwezi September mwaka huu. Mara ya mwisho kushudia Zlatan kucheza mechi sita za ligi bila kufunga ilikuwa December mwaka 2007 alipokuwa kwenye klabu ya Inter Milan ya Italia. Man Utd ilitoka suluhu dhidi ya Burnley nyumbani, huku mlinda malango wa Burney aliibuka shujaa kwa kuokoa mashuti kumi na moja. Namba 10 (Tottenham Hotspurs, Westbrom) Sare ya 1-1 dhidi ya mabingwa wa msimu uliopita Leicester City umeifanya timu ya Tottenham Hotspurs kucheza mechi kumi bila ya kufungwa. Mara ya mwisho kwa Spurs kufanya hivyo ikiuwa ni msimu wa 1990/91. Hadi sasa Spurs wamecheza mechi kumi, kushinda mechi tano na kutoka sare mara tano. (w5 D5, L0) matokeo ambayo yanaifanya Spurs kuwa timu pekee ambayo hajipoteza mchezo msimu huu. Klabu ya Westbrom imepoteza michezo yote kumi ya hivi karibuni ambayo timu hiyo imecheza dhidi ya Man City. Wikiendi iliyopita Westbrom waliwa nyumbani walifungwa na Man City 4-0

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni