pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumatano, 26 Oktoba 2016
AZAM FC Yamtosa Hans van der Pluijm Yasema Hatuamini kupata kitu kipya kutoka kwa Hans
Baada ya Hans van Pluijm kujiuzulu kuifundisha klabu ya Yanga zikaanza kuenea taarifa kwamba matajiri wa ligi ya Tanzania bara klabu ya Azam FC inamuhitaji mholanzi huyo aliyeisaidia Yanga kupata mafanikio katika kipindi chake kama kocha mkuu wa timu hiyo.
Uongozi wa Azam FC umetoa ufafanuzi juu ya taarifa hizo ambazo tayari zilianza kumhusisha kocha huyo kutua Chamazi kufatia mfululizo wa matokeo mabovu ya benchi jipya la ufundi la Azam linaloongozwa na Zeben Hernandez.
“Sisi tunakocha wetu ambaye anamkataba ambao bado anautumikia, tulishasema toka mwanzo matokeo ya uwanjani na benchi letu la ufundi sio tatizo hivyo tupo tayari kuvumilia na kuendelea na mwalimu wetu akiendelea kujifunza na kuona mpira wetu utakuwa namna gani hatuna hesabu za kumbadilisha kocha sasahivi,” amekaririwa ofisa mtendaji mkuu wa Azam FC Saad Kawemba wakati anazungumza na kituo kimoja cha radio.
“Hata kama itatokea tukaamua kubadilisha kocha hatuna sababu ya kuchukua kocha kutoka kwenye klabu nyingine za hapa nyumbani. Sisi tunaimani kwamba kocha tuliyenae anatosha, wachezaji wanajukumu la kumwelewa mwalimu licha kwamba inaweza kuchukua muda kuelewa falsafa zake.”
“Tumecheza na Yanga chini yake (Hans) mechi nyingi, lakini nyingi zimekuwa sare ushindi tumekuwa karibu sawa kwahiyo hatuamini kama tutapata kitu kipya kutoka kwake. Tunamuheshimu ni kocha mzuri, tunamtakia kilalaheri, tunasikitika kwanini kaondolewa katikati ya ligi kama viongozi tunamuheshimu na tunaheshimu falsafa zake na ufundishaji wake lakini kwa sasa Azam tupo complete.”
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni