Jumamosi, 29 Oktoba 2016

LIVE KUTOKA KAMBARAGE SHINYANGA: MWADUI FC 0 VS 2 SIMBA (MAPUMZIKO)

MAPUMZIKO GOOOOOOOOO Dk 45, Kichuya anaifungia Simba bao la pili leo, la nane kwake akiunganisha pasi safi ya Mohamed Ibrahim Dk 44, Rajab Ismail anaingia vizuri hapa, anapiga shuti hatari. Lakini linatoka kidogo tu nje ya lango la Simba SUB Dk 42, Simba wanafanya mabadiliko, wanamtoa Mavugo na nafasi yake inachukuliwa na Ame Ali Dk 40 sasa, bado mpira haujachangamka sana, Simba wana mashambulizi kadhaa lakini si makini katika umaliziaji na MWadui FC wanaonekana kutokuwa na mipango bora wanapofika kwenye lango la Simba Dk 35, hatari kwenye lango la Mwadui, Kazimoto anamtoka kipa na kumpa Muzamiru pasi peke yake na nyavu, anaukosa mpira unaokolewa DK 33, Mwadui wanaingia vizuri, shuti la Madenge lakini linamgonga Angban usoni na Mwanjale anaokoaGOOOOOO Dk 32, Mo Ibrahim anamchambua beki wa MWadui na kufunga bao safi kabisa kwa Simba Dk 31, pasi nzuri ya Kazimoto, Mo Ibrahim anashindwa kuitumia na kupiga shuti nyanya hapa Dk 29, MWadui wanapata kona ya kwanza hapa, inachongwa vizuri na Rashid Ismail anajitwika lakini inakuwa ni goal kick Dk 25, Mavugo anatoa krosi safi kabisa kwa Kichuya, lakini anaruka na kupiga kichwa juuuu Dk 22 sasa, mpira hauvutii sana, hakuna timu inayoonyesha imepania kupata mabao ya haraka. Zaidi mpira unachezwa katikati ya uwanja na hakuna mashambulizi makali Dk 14, Rashid Ismail anapiga shuti karibu kabisa na langu la Simba, unapita juu Dk 9 Mwadui wanapoteza nafasi nyingine ya wazi hapa baada ya kupiga shuti kuuubwa Dk 9, MWadui wanagongeana vizuri wanafunga hapa lakini Hamisi alikuwa ameishaotea Dk 7, Mavugo tena anaichezea nafasi nyingine na kupiga juu akiwa na nafasi nzuri kama angetulia Dk 6, Mavugo anawachambua mabeki wa Mwadui na kuachia mkwaju mkali, unatoka juu kidogo Dk 4, bado hakuna kitu chochote ambacho kinaonekana ni mabadiliko kwa kuwa mpira zaidi unachezwa katikati ya uwanja. Dk 1 Simba wameanza kwa kasi lakini shuti la Mavugo linatoka nje. 1. Vicent Angban 2. Janvier Bukungu 3. Mohamed Zimbwe 4. Method Mwanjale 5. Juuko Murshid 6. Jonas Mkude 7. Mzamiru Yassin 8. Mwinyi Kazimoto 9. Laudit Mavugo 10. Shiza Kichuya 11. Mohamed Ibrahim Sub Manyika Hamadi Novart Ndemla Ndusha Ajib Ame

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni