pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumamosi, 29 Oktoba 2016
LIVE KUTOKA KAMBARAGE SHINYANGA: MWADUI FC 0 VS 1 SIMBA
Dk 35, hatari kwenye lango la Mwadui, Kazimoto anamtoka kipa na kumpa Muzamiru pasi peke yake na nyavu, anaukosa mpira unaokolewa
DK 33, Mwadui wanaingia vizuri, shuti la Madenge lakini linamgonga Angban usoni na Mwanjale anaokoaGOOOOOO Dk 32, Mo Ibrahim anamchambua beki wa MWadui na kufunga bao safi kabisa kwa Simba
Dk 31, pasi nzuri ya Kazimoto, Mo Ibrahim anashindwa kuitumia na kupiga shuti nyanya hapa
Dk 29, MWadui wanapata kona ya kwanza hapa, inachongwa vizuri na Rashid Ismail anajitwika lakini inakuwa ni goal kick
Dk 25, Mavugo anatoa krosi safi kabisa kwa Kichuya, lakini anaruka na kupiga kichwa juuuu
Dk 22 sasa, mpira hauvutii sana, hakuna timu inayoonyesha imepania kupata mabao ya haraka. Zaidi mpira unachezwa katikati ya uwanja na hakuna mashambulizi makali
Dk 14, Rashid Ismail anapiga shuti karibu kabisa na langu la Simba, unapita juu
Dk 9 Mwadui wanapoteza nafasi nyingine ya wazi hapa baada ya kupiga shuti kuuubwa
Dk 9, MWadui wanagongeana vizuri wanafunga hapa lakini Hamisi alikuwa ameishaotea
Dk 7, Mavugo tena anaichezea nafasi nyingine na kupiga juu akiwa na nafasi nzuri kama angetulia
Dk 6, Mavugo anawachambua mabeki wa Mwadui na kuachia mkwaju mkali, unatoka juu kidogo
Dk 4, bado hakuna kitu chochote ambacho kinaonekana ni mabadiliko kwa kuwa mpira zaidi unachezwa katikati ya uwanja.
Dk 1 Simba wameanza kwa kasi lakini shuti la Mavugo linatoka nje.
1. Vicent Angban
2. Janvier Bukungu
3. Mohamed Zimbwe
4. Method Mwanjale
5. Juuko Murshid
6. Jonas Mkude
7. Mzamiru Yassin
8. Mwinyi Kazimoto
9. Laudit Mavugo
10. Shiza Kichuya
11. Mohamed Ibrahim
Sub
Manyika
Hamadi
Novart
Ndemla
Ndusha
Ajib
Ame
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni