Mkurugenzi mkuu wa Juventus Giuseppe Marotta amethibitisha kwamba wakala wa Paul Pogba atalipwa kiasi cha 27 million euros ($30 million) kama malipo yake kutoka kwenye uhamisho wa Pogba kwenda Manchester United.Pogba alirejea United mwezi August kwa rekodi ya uhamisho iliyovunja rekodi ya $116 million. Marotta alikaririwa na vyombo vya habari vya Italia akiongea katika mkutano wa wenye hisa wa klabu Jumanne iliyopita akisema kwamba “27 million (euros) zitalipwa kwa wakala wa Pogba Mino Raiola. Hivyo kiasi kitakachobaki upande wetu ni 72 million ($78 million)” baada ya makato yote.Marotta amesema kwamba Pogba alijiunga na Juve kutoka United 2012 kwa uhamisho kwa ada ya 1.5 million euros ($1.6 million). Marotta ameongeza kwamba usajili wa mkopo wa miaka miwili wa Juan Cuadrado kutoka Chelsea utaigharimu 5 million euros ($5.4 million) kwa msimu na endapo Juventus watashinda Serie A msimu huu basi watapaswa kumsajili Cuadrado kiujumla kwa kulipa 20 million ($22 million)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni