pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumatatu, 24 Oktoba 2016
BAADA YA HANS VAN DER PLUIJM KUMWAGANA NA YANGA MWAMBUSI ATAIONGOZA YANGA KWA MUDA, LWANDAMINA ATAANZA KAZI MWEZI UJAO
Kocha Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi atakiongoza kikosi cha Yanga katika mechi zilizobaki hadi hapo kocha mkuu mpya atakapoanza kazi.
Taarifa za ndani kutoka Yanga zinasema George Lwandamina raia wa Zambia ataanza kazi rasmi Novemba Mosi.
Tayari Lwandamina yuko jijini Dar es Salaam na Kocha Hans van der Pluijm ameachia ngazi rasmi kuinoa Yang.
“Mwambusi ndiye ataendelea na kikosi, mambo mengine yakikamilika Lwandamina ataanza kazi,” alisema.
Awali ilielezwa kwamba Pluijm atakuwa ni Mkurugenzi wa Ufundi wa Yanga kabla ya mwenyewe kuamua kujiuzulu.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni