Jumatano, 26 Oktoba 2016

Kama ujui nakwambia Yanga ndio habari ya mjini kwa sasa Tiboroha afunguka baada ya Hans van Pluijm kujiuzulu Yanga

Aliyekua Katibu Mkuu wa Young Africans Jonas Tiboroha ameshangazwa na maamuzi ya uongozi wa klabu hiyo ya kutafuta kocha mwingine na kubariki maamuzi ya kujiuzulu yaliyochukuliwa na Hans van der Pluijm. Tiboroha amesema kuondoka kwa kocha Hans van Pluijm huenda likawa pigo kubwa kwa kikosi cha Yanga ambacho bado kinahitaji huduma yake, kutokana na kuwa na rekodi nzuri ya kuvutia tangu alipokuja nchini miaka miwiwli iliyopita. “Nilikuwa siamini lakini naona inatokea, nilikuwa siamini kwasababu najaribu kuitathmini klabu ya Yanga kwa miaka miwili kama kuna watu hawatunzi kumbukumbu vizuri, niwakumbushe kwenye ligi msimu uliopita hadi sasa hivi hii ni timu ambayo imepoteza mechi mbili.” “Kwa mechi zilizochezwa hadi sasahivi, Yanga ni ya pili katika msimamo wa ligi naona timu bao inafanya vizuri katika ligi. Kitu ambacho nilitegemea klabu ya Yanga inegafanya hususan katika dirisha la usajili lililopita kuna sehemu ambazo hata wakati bado nipo Yanga zilikuwa ni sehemu ambazo hata mwalimu ukimuuliza alikuwa anazitaja.” “Msimu umepita hakuna kilichofanyika katika hizo sehemu badala yake nimeona kuna wachezaji wamekuja lakini mimi sikuona kama ni kipaumbele kwa hao wachezaji kwasababu nafasi hizo zilikuwa na wachezaji wa kutosha.” “Unaongeza kiungo wa pembeni wakati Yanga inawachezaji karibu watatu katika nafasi hiyo, walinzi wa pembeni kulia Yupo Juma Abdul na Mbuyu Twite pia anaweza kucheza nafasi hiyo, upande wa ulinzi wa kushoto hakuna tatizo.” “Sehemu ambayo tulikuwa tunahitaji mtu kwa muda mrefu ni mchezaji wa kati ambaye atasaidia kukaba, hatuna defensive midfielder kwa muda mrefu sana. Kwa timu ambayo imekuwa ikishiriki mashindano makubwa mara nyingi hiyo sehemu imekuwa dhaifu kwenye matokeo ya Yanga.” “Sijaona matatizo makubwa sana kwa Hans ukilinganisha na walimu wengine ambao wamekuwepo hapa nchini na hata katika timu ambazo tumecheza nazo umeona kabisa tofauti ilikuwa ni ndogo na tofauti si ya ufundi isipokuwa imekuwa ni tofauti ya organization ya wachezaji wenyewe.” “Mimi sijui labda zipo sababu za msingi zilizowafanya wabadili benchi la ufundi ambazo siwezi kuzisemea kwasababu sipo ndani, siyo mjumbe wa kamati ya mashindano lakini siyo mjumbe wa kmati ya utendaji ya Yanga kiasi cha kujua nini kinaendelea.”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni