Jumatatu, 31 Oktoba 2016

MASHALI AMEUWAWA SIKU CHACHE BAADA YA KUBADILI DINI NA KUWA MWISLAMU, ALIKUWA AKIITWA MOHAMMED

Wapenda ngumi nchini wako katika majonzi makubwa baada ya kifo cha bondia nyota, Thomas Mashali. Mashali ameuwawa katika moja ya viunga vya jiji la Dar es Salaam, ikielezwa aliokotwa eneo la Kimara ingawa kuna wengine wanasema ameokotwa eneo la Tabata. Kitu ambacho Watanzania wengi hawakukijua ni kwamba, wakati mauti yanamkuta, Mashali alikuwa amebadili dini siku chache, kutokuwa kuwa Mkristo hadi Mwislamu, akaamua kuacha kutumia jina la Thomas na alikuwa akitumia jina la Mohammed. Katibu Mkuu wa Shirikisho la Ngumi za Kulipwa (PST), Anthony Rutta amesema, Mashali kweli alibadili dini. "Kweli alikuwa anaitwa Mohammed, hili alitueleza mwenyewe kwamba aliamua mwenye kwa hiari yake kuwa mwislamu," alisema Rutta.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni