Ijumaa, 28 Oktoba 2016

BOCCO AIOKOA AZAM FC MWISHONI, YAITWANGA KAGERA SUGAR KAITABA

Azam FC imezinduka mwishoni na kuichapa Kagera Sugar kwa mabao 3-2 katika mechi ya Ligi Kuu Bara. Katika mechi hiyo kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, Kagera walionekana kama watashinda mechi hiyo baada ya kutangulia mapema. Lakini Azam FC iliyokuwa ikicheza bila ya kiungo wake Himid Mao aliyekuwa na kadi nyekundu ilisawazisha kupitia kwa Mudathir Yahya, baadaye ikasawazisha mara nyingine kupitia Frank Domayo. Nahodha, John Raphael Bocco alimaliza kazi jioni kabisa na kuwaacha Kagera wakishangaa. Hiyo ni mechi ya pili, Kagera Sugar wanaambulia kipigo katika uwanja wao wa nyumbani..

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni