Alhamisi, 27 Oktoba 2016

Mwambusi ameuongelea ushindi wa kwanza akiwa Mkuu wa Benchi la Ufundi Yanga

Kocha Mkuu wa muda wa klabu ya Yanga SC Juma Mwambusi amepongeza wachezaji wake kwa kile walichofanya kwenye mchezo wa jana dhidi ya wanajeshi wa JKT Ruvu baada ya kuwashushia kipigo cha mabao 4-0. Mwambusi ambaye anashikilia nafasi hiyo baada ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo Hans van der Pluijm amesema ilikuwa ni lazima wapate ushindi kwa udi na uvumba kutokana na hali iliyopo klabuni humo kwa sasa. “Mimi nawashukuru wachezaji kwa sababu kwa hali ilivyo ilikuwa ni lazima tupate matokeo ya ushindi, tumepata pointi tatu, tumeweza kucheza na timu ya JKT ambayo ni ngumu na bora,” alisema. Amewapongeza wapinzani wao kwa kuwapa wakati mgumu hasa katika kipindi ha kwanza hali iliyopelekea kubadili mbinu kipindi cha pili ili kupata matokeo bora zaidi. “Niwapongeze kwasababu kipindi cha kwanza walitupa ugumu ambao ulipelekea kuweza kukosa kuongoza kwa magoli ya kutosha, lakini tulipata goli moja na kipindi cha pili tuliweza kubadili mbinu na kubaini udhaifu wao na kuutumia na tukaweza kupata magoli matatu. Pia amewapongeza wachezaji wake kwa kutekeleza kwa ufanisi kwa yale aliyowalekeza bila kusahau mashabiki na wapenzi wa klabu hiyo kwa sapoti kubwa waliyowapa wakati wakiwa uwanjani. “Kwa hiyo niwapongeze wachezaji wangu kwaababu ya kushika maelekezo na kuweza kuyafanyia kazi, na pia vilevile tuwashukuru Wanayanga wote kwa ujumla kutokana na ushirikiano waliotupa na kufanikisha kupata ushindi huu.” Yanga kwa sasa wanashika nafasi ya pili wakiwa na alama 24 nyuma ya vinara Simba wenye alama 29.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni