pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Alhamisi, 27 Oktoba 2016
Washambuliaji wanne Yanga wamefunga magoli 20 kati ya 24…’
Na Baraka Mbolembole
Amis Tambwe alifunga mara mbili katika ushindi wa Yanga SC 4-0 JKT Ruvu siku ya jana, magoli yake hayo mawili yamemfanya kufikisha jumla ya magoli 6 msimu huu na kukaa juu kiufungaji katika timu yake.
Kiungo mshambuliaji, Saimon Msuva licha ya kusaidia upatikanaji wa magoli tisa kwa wachezaji wenzake, naye alifunga goli lake la tano katika ligi kuu Tanzania Bara.
Msuva ni mfungaji bora wa VPL msimu wa 2014/15 na Tambwe alishinda tuzo hiyo msimu uliopita.
Wawili hao wamefunga jumla ya magoli 11 msimu huu na jambo lingine la kuvutia katika timu hiyo ni washambuliaji wengine wawili kufunga jumla ya magoli 9.
Mzambia, Obrey Chirwa alifunga pia katika ushindi vs JKT Ruvu. Chirwa amefunga magoli matano katika game tano mfululizo za Yanga na Mzimbabwe, Donald Ngoma yeye tayari amefanikiwa kufunga magoli manne.
Kiujumla wanne hao (Tambwe, Msuva, Chirwa na Ngoma) wamekwisha funga magoli 20 katika VPL kufikia game ya 11. Ikiwa na magoli 24 katika mechi 11 Yanga ndio timu iliyofunga magoli mengi zaidi katika ligi hadi sasa.
Kiungo wa pembeni, Deus Kaseke yeye amefanikiwa kufunga magoli matatu huku goli moja likifungwa na kiungo, Juma Mahadhi.
USHIRIKIANO Safu hii ya mashambulizi ya Yanga imekuwa ikicheza kwa ushirikiano mkubwa uwanjani na jambo hilo limewafanya kutengenezea nafasi nyingi za kufunga.
Kwa mwenendo wao huo wanaweza kufunga magoli katika kila mchezo na kuendelea kuibeba timu yao.
Yanga itacheza na Mbao FC mwishoni mwa wiki hii kisha wataelekea Mbeya kucheza na Tanzania Prisons kisha Mbeya City FC wiki ijayo.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni