pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumanne, 25 Oktoba 2016
Mapya yaibuka dili la Farid Musa na Tenerife
Farid Musa bado anaendelea kuonekana nyumbani wakati tuliambiwa dili lake lilishakamilika kwenda kucheza soka la kulipwa kwenye klabu ya Tenerife nchini Hispania, lakini kitendo cha Faird kuendelea kuonekana Bongo kinaendelea kuzua maswali mengi kwa wadau wa soka nchini hali iliyopelekea nahodha wa timu taifa ya Tanzania Mbwana Samatta kuhoji kitu gani kinachokwamisha mchakato huo.
Wakala wake John Sonzano anasemaje?
“Mkataba wa Farid Musa uliopo na unaotambulika kwa sasa kutoka Azam kwenda Tenerife ni mkataba wa mkopo, hili liwekwe wazi kwa watanzania wote ili waelewe kwamba hajauzwa bali ametolewa kwa mkopo.”
“Changamoto zilizopo ni za vibali vya Farid kufanya kazi Hispania lakini tuanaamini kabla ya mwisho wa mwaka huu kila kitu kitakuwa tayari ili akaitumikie Club Deportivo Tenerife kwa mkopo.”
Msimamo wa Azam FC
“Hakuna mtu ambaye amemzuia Farid na sisi hatujafanya jambo lolote kuonesha tunamzuia mchezaji. Kila mmoja kwenye timu kuanzia Kurugenzi, Executive Directors pamoja na viongozi wa timu wote ambao ni watendaji wa kilasiku tunafanya juhudi za dhati kuhakikisha Farid anakwenda Hispania,” anasema meneja mkuu wa Azam FC Abdul Mohamed.
“Tumeishi Ulaya tumeona namna kazi zinavyofanyika hasa katika suala la kupata kibali cha kufanya kazi hapo ndipo pamekuwa na ukwamo kwasababu issue ya Farid ipo complicated kwenye suala la kupatikana kwa kibali cha kazi.”
“Wanaotoa kibali cha kufanya kazi sio Azam FC ni mamlaka ya uhamiaji ya Hispania hasa kwa klabu ya Tenerife ambayo lazima wapeleke documents ambazo ni sahihi Farid kupewa kibali cha kazi ili aweze kuingia Hispania kufanya kazi.”
“Sisi Azam pamoja na ubalozi wa Hispania hapa Tanzania tumemaliza nafasi yetu kilichobaki sasahivi ni upande wa Tenerife waweze kumalizia ili Farid aondoke.”
“ITC ya Farid imeshatumwa, kama tungekuwa tunamuhitaji, tungewaambia wairudishe ili tuendelee kumtumia Farid kwasababu bado yupo anafanya mazoezi na sisi bado anamkataba na sisi na tunamlipa mshahara.”
Sheria za kufanya kazi kwenye kisiwa cha Tenerife
Kisiwa ambacho ndipo yanapopatikana makazi ya Club Deportivo Tenerife Tenerife wao wanasheria na taratibu zao za kufanya kazi kwa watu ambao sio wakazi wa eneo hilo tofauti na sheria za kawaida za nchini Hispania.
Wanataka kupata documents zilizokamilika kwamba dili kati ya Azam na Tenerife limekamilika, kilakitu kikiwa tayari, karatasi za makubaliano zinakwenda kwenye mamlaka husika kwa ajili ya wao kuanza au kutoa kibali cha Farid kwenda kufanya kazi.
Makubaliano ya Azam na Tenerife
Inasemekana, pamoja na dili hilo kufikiwa kwamba Farid anakwenda Tenerife kwa mkopo lakini dili hilo linakwama kutokana na makubaliano binafsi ya vipengele vilivyomo kwenye mkataba.
Kulikuwa na machaguo mawili, kumuuza moja kwa moja ambapo Azam walitaka walipwe euro 600,000 lakini pia bado walitaka 50% endapo Farid atauzwa kutoka Tenerife kwenda klabu nyingine kitu ambacho Tenerife waliona ni kigumu wakaamua kuchukua chaguo la pili ambalo ni kumchukua kwa mkopo.
Akichukuliwa kwa mkopo Tenerife hawalipi ada yoyote ya uhamisho lakini bishara ikifanyika kwa mara kwanza, Azam wanataka 50%, Farid akiuzwa mara ya pili Azam wanataka 30% akiuzwa kwa mara ya tatu Azam wanataka wapate 20%.
Tenerife wakaona bado vipengele ni vigumu na mlolongo ni mrefu. Kwahiyo bado vilabu vinaendelea kukubaliana na hiyo ndiyo sababu kubwa inayochelewesha dili la Farid.
Tuendelee kusubiri kuona kama Azam naTenerife watafikia makubaliano ili Farid akacheze soka barani Ulaya.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni