pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumapili, 30 Oktoba 2016
Mayanja ameitaja sababu ya kumtoa Mavugo katikati ya kipindi cha kwanza Mwadui vs Simba
Inawezekana kabisa kuna watu walishangazwa kumshuhudia mshambuliaji wa Simba Laudit Mavugo akipumzishwa katikati ya kipindi cha kwanza na nafasi yake kuchukuliwa na Ame Ali ‘Zungu’ katika mechi ya Mwadui 0-3 Simba, mara baada ya game hiyo kumalizika nikamtafuta kocha msaidizi wa Simba Jackson Mayanja kutoa sababu ya benchi la ufundi kumpumzisha Mavugo.
Mayanja amesema Simba haitegemei mchezaji mmoja, kikosi kimesimama vizuri ndiyo maana kwenye mchezo wao dhidi ya Mwadui, Ibrahim Mohamed amefunga magoli mawili.
Kuhusu kumpumzisha Mavugo, Mayanja amesema: “Kama mchezaji hafanyi vizuri unamtoa anaingia mwingine kuchukua nafasi ili abadili mchezo,” alisema Mayanja muda mchache baada ya kumalizika kwa mechi ya Mwadui vs Simba.
Mechi iliyopita ya Simba dhiti ya Toto Africans, Mavugo alianzia benchi lakini aliingia kipindi cha pili baada ya Fredrick Blagnon kuumia na kushindwa kuendelea na mchezo. Mavugo alifunga goli moja kwenye ushindi wa Simba 3-0 Toto Africans.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni