Ijumaa, 28 Oktoba 2016

Yanga yawaponza wachezaji Kagera Sugar, wasimamishwa kwa tuhuma za upangaji matokeo

Uongozi wa Kagera Sugar umewasimamisha wachezaji wake wawili golikipa Hussein Sharif ‘Casillas’ na beki Erick Kyaruzi kwa tuhuma za kuihujumu timu wakati wa mchezo wa liopoteza kwa kufungwa magoli 6-2. Katibu Mkuu wa klabu hiyo Hamisi Madaki amethibisha kuwasimamisha wachezaji hao kwa muda usiojulikana kwa ajili ya kupisha uchunguzi juu ya tuhuma zinazowakabili. “Tunaendelea na uchunguzi kwasababu kunaonekana kulikuwa na hujuma katika mechi yetu na Yanga kwahiyo tumeona tuendelee na uchunguzi na tumeona wakae kando wakati tunaendelea na uchunguzi huo.” “Aina ya magoli tuliyofungwa kila mtu aliyaona na yanatia wasiwasi mkubwa. Suala sio idadi ya magoli suala ni aina ya amagoli mtu aliayofungwa, hata kama ni goli moja lakini kama linatia wasiwasi lazima tuchukue hatua.” “Makosa ya namna ile hatukuridhika nayo ndiyo maana tunafanya uchunguzi. Hata beki goli alilofungisha unaona dhahiri kwamba halikupashwa kuwa goli ndiyo maana tunafanya uchunguzi.” “ nikiwa kama Mtendaji mkuu wa klabu, hiyo taarifa sina sisi tumewasimamisha na hata barua tulizowaandikia tumesema tumewasimamisha . Suala la kuwaondoa kabisa hilo siwezi kulisemea, taarifa nilitoa mbele ya wachezaji na benchi la ufundi baada ya kukaa viongozi na benchi la ufundi tulikubaliana kuwasimamisha.” “Tumewasimamisha kwa muda usiojulikana mpaka tukamilishe uchunguzi, hii si mara ya kwanza watu wanasahau historia, tumeshawahi kusimamisha wachezaji na kuwafukuza kabisa hapo kabla.” Katika mchezo huo, Hussein Sharif alifungwa magoli matatu kipindi cha kwanza kabla ya kufanyiwa mabadiliko kumpisha David Burhani ambaye pia alifungwa magoli matatu. Kyaruzi yeye alirudisha pasi fupi kwa golikipa wake ambapo Donald Ngoma aliuwahi mpia huo na kufunga bao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni