Alhamisi, 27 Oktoba 2016

Mapya yaibuka Wakala wa Farid Musa akanusha kupatikana kibali cha kazi, mchakato bado unaendelea…

Jana usiku Azam TV kupitia kipindi cha MSHIKEMSHIKE VIWANJANI walithibisha kupatikana kwa kibali cha kazi cha kiajana Farid Musa kwa ajili ya kwenda kucheza soka la kulipwa kwenye klabu ya Tenerife ya nchini Hispania, lakini General Manager wa Azam FC Abdul Mohamed alisikika kwenye radio akithibisha kupokea kibali cha kazi cha winga huyo ambaye kwa sasa hajacheza mechi yoyote ya kiushindani tangu kuanza kwa ligi akisubiri safari yake kuelea Ulaya. Uchunguzi uliofanywa na shaffihdauda.co.tz umebaini kuwa, habari iliyotoka Azam FC kuhusu kupokea kibali cha kazi cha Farid Musa si za kwelibadala yake wamepokea form ya kuombea kibali hicho. Wakala wa Farid Musa, John Sorzano amekanusha habari zilizozagaa kuwa tayari kibali cha kazi kimeshatoka na badala yake amesema hicho kilichotapakaa kwenye mitandao ya kijamii si kibali ni form ambayo itatumiwa katika mchakato wa kuombea kibali. Solzano ameshangaa form hiyo kutapakaa mitandaoni wakati ni kitu cha siri huku akisisitiza kuwa, wametumiwa Azam na yeye lakini kwa upande wa Tanzania, tayari form hiyo imeshaonekana kwenye mitandao ya kijamii. Kitendo cha hiyo form kusambaa mitandaoni huenda kukahatarisha Farid kupata kibali cha kazi. “Hii form nimetumiwa mimi pamoja na klabu ya Azam, lakini nashangaa wao wameiweka mitandaoni wakati ni kitu cha siri, kwa upande wangu mimi nilifanya kuwa siri. Farid sio kwamba amepata kibali lakini mchakato bado unaendelea,” anasema John Sorzano wakala wa Farid Musa. “Kitendo cha kuitoa form hadharani ambayo ni document ya serikali kinaweza kikahatarisha mchakato kwasababu ikumbukwe Tanzania pia kuna ubalozi wa Hispania ambao unaweza kuona yanayofanyika kwenye mitandao ya kijamii wanaweza wakahoji kwanini document hiyo imesambaa hivyo, inaweza kuleta ugumu.”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni