pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumatatu, 24 Oktoba 2016
Neno la mwisho la Hans van Pluijm kwa mashabiki wa Yanga
Kocha Mkuu wa Yanga Hans van der Pluijm amethibisha kukabidhi barua ya kujiuzulu kwa uongozi wa Yanga baada ya kusambaa kwa taarifa za ujio wa kocha mpya mzambia George Lwandamina ambaye atachukua mikoba ya Hans.
Pluijm amefikia hatua hiyo baada ya kusikia klabu ipo kwenye mchakato wa kumwajiri kocha mpya ikiwa yeye kocha aliyepo madarakani hana taarifa yoyote rasmi lakini taarifa tayari inajulikana.
Mholanzi huyo amewashurukuru mashabiki wa Yanga kwa kumuunga mkono katika kipindi chote akiwa kocha wa timu yao lakini amesisitiza imebidi achukue uamuzi huo kutokana na hali ilivyo sasa ndani ya klabu.
“Nili kweli nimejiuzulu, nilifanya maamuzi Jumamosi baada ya mechi yetu dhidi ya Kagera Sugar na tayari nimekabidhi barua yangu kwa uongozi. Ninasababu zangu za kufanya hivyo, kama unataka kujua sababu waulize klabu sihusiki katika hilo sina mamlaka ya kutolea ufafanuzi, sitaki kuleta mgongano kati ya klabu na mimi kwasababu mimi ni mtu ninayeheshimika unapaswa kujua hilo. Ninajiheshimu na ninajua kuheshimu wengine.”
“Nawashukuru mashabiki kwa ushirikiano wao wa nguvu walionipa, nimekuwa nikiwaheshimu siku zote. Nawaomba wanisamehe kwa uamuzi niliochukua, sikuwa na namna nyingine zaidi ya kufanya hivyo.”
Inadaiwa kunawakati kulitokea kutoelewana kati ya Van Pluijm na uongozi wa klabu ya Yanga baada ya uongozi wa juu kutoa shinikizo kwa kocha huyo kumsajili Mrisho Ngasa baada ya kuvunja mkataba na klabu ya Free State Stars ya Afrika Kusini.
Hans aliwaambia viongozi hao kwamba, Ngasa si mchezaji mbaya, lakini kwa sasa simuhitaji. Ujio wa Ngasa kwenye timu utasababisha mvurugano kwenye timu, Simon Msuva, Juma Mahadh, Deus Kaseke na Geofrey Mwashiuya ni vijana wanne wanaocheza nafasi sawa na Ngasa, ujio wa Ngasa kwenye timu kama mchezaji mwenye jina tayari kutaharibu mipango ya timu.
Habari za ndani ya Yanga zinazidi kusema kuwa, katika mchezo wa watani wa jadi (October 1, 2016 Yanga 1-1 Simba) inasemekana kuna baadhi ya wachezaji walicheza bila matakwa ya benchi la ufundi huku wengine wakiwekwa benchi kwa shinikizo la baadhi ya viongozi wa juu.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni