MPIRA UMEKWISHAAAA
GOOOOOOOOO Dk 90, anawavizia kipa na beki wa JKT na kuandika bao la nne
SUB Dk 89, Mahadhi anaingia kuchukua nafasi ya Msuva
Dk 86 mpira unaonekana kupunguza kasi kwa kiasi kikubwa, huenda Yanga wameridhika na JKT wameishakata tamaa kwamba hawawezi kurudisha tatu zote kwa dakika nne zilizobaki
SUB Dk 84, Kaseke anakwenda benchi na nafasi yake inachukuliwa na Geofrey Mwashiuya
GOOOOOOOO Dk 83, Msuva anapachika bao safi kabisa akiunganisha pasi nzuri ya Tambwe
KADI Dk 80 Kamusoko analambwa kadi ya njano kwa kumzonga Michael Aidan
KADI Dk 77, Yondani analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Samwel Kamuntu
Dk 69 hadi 74, mpira unachezwa zaidi katikati ya uwanja na hakuna madhara makubwa kwenye malango
Dk 68, Nurdnin Mohammed analambwa kadi ya njano baada ya kuunganisha hadi wavuni mpira kwa kutumia mkono wake
GOOOOOOO Dk 61, Tambwe anafunga bao safi kabisa akiwa ametulia baada ya mabeki wa JKT kumsahau
KADI Dk 61, Nashon Naftal analambwa kadi ya njano kwa kumrukia Mwinyi
SUB Dk 60, Michael Aidan anaingia kuchukua nafasi ya Kindamba ambaye ameumia baada ya kugongwa na Mwinyi
wa Yanga
Dk 59, Kindamba anatolewa nje baada ya kufanyiwa huduma ya kwanza, inaonekana amechanika kichwani
KADI Dk 57, Mwinyi analambwa kadi ya njano baada ya kumgonga kichwani mchezaji wa JKT, Omary Kindamba anayetibiwa
SUB Dk 56, Yanga wanafanya mabadiliko yao ya kwanza, wanamtoa Ngoma na nafasi yake inachukuliwa na Amissi Tambwe
Dk 54, Yanga wanagongeana vizuri, Haji Mwinyi anapiga krosi matata kabisa lakini Msuva anaunganishwa kwa kichwa cha mwendokasi
Dk 52, Chirwa tena, akiwa hatua tatu kutoka alipo kipa wa JKT lakini anashindwa kuunganisha mpira
Dk 46 kipindi cha pili kimeanza, Yanga wakiwa wanapeleka mashambulizi yao Kusini na JKT wanasukuma Kaskazini
MAPUMZIKO
DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 45, JKT wanapata kona lakini haina mafanikio
Dk 44 Yanga wanapoteza wanapotez anafasi nyingine tena ya wazi hapa baada ya Msuva kuukosa mpira
KADI Dk 39 kadi ya kwanza katika mchezo huu inatoka, Kassim Kisengo wa JKT anazawadiwa baada ya kumuangusha Chirwa
Dk 37, nafasi nyingine kwa Yanga, Ngoma akiwa hatua tano na kipa, anapiga kichwa pembeni juuuuuu
Dk 35, krosi safi ya Kessy, Ngoma anabaki na kipa, anampa mikononi
Dk 34 Chirwa anawahadaa mabeki wa JKT, anapiga shuti safi kabisa, lakini kipa anapangua na mabeki wanaosha
Dk 30, yuko chini anatibiwa baada ya kugongwa na beki wa JKT wakati akiokoa mpira, anatoka nje na baadaye mwamuzi anamruhusu kuendelea na mchezo
Dk 29, Kessy anaachia shuti kali tena, lakini mpira unawababatiza mabeki wa JKT na kuokoa
Dk 27 sasa, Yanga ndiyo wanaonekana kumiliki zaidi mpira katikati ya uwanja lakini hakuna shambulizi kubwa hata moja
Dk 22, Atupele anampa Dilunga pasi safi kabisa lakini shuti lake, mpira unatoka sentimeta chache nje ya lango la JKT
Dk 19, Kessy anapiga mpira unakwenda moja kwa moja na kugonga mwamba wa juu, mabeki JKT wanaokoa
Dk 12, Kamusoko naye anashindwa kuukwamisha mpira wavuni akiwa amebaki na kipa. Yanga wanazichezea hizi nafasi na wanapaswa wawe makini sana
Dk 11, Yanga wanafanya shambulizi jingine, mpira unamfikia Chirwa akiwa na kipa peke yake, lakini anampa mikononi
Dk 10, Kaseke anawahadaa mabeki JKT na kutoa pasi safi kwa Msuva lakini anapiga shuti kuuubwaaaa
Dk 8, JKT wanachonga kona yao ya pili lakini mpira unaokolewa mbali kabisa na Yondani
Dk 7, Atupele Green anaingia vizuri na kuachia shuti kali, Yondani anazuia na kuwa kona, inapigwa inakuwa nje tena, kona
GOOOOOO DK 6 Chirwa anaifungia Yanga bao kwa shuti kali baada ya beki wa JKT kuanguka na kuuacha mpira nyuma, MSuva akauwahi na kumpa Chirwa ambaye amemaliza kazi
Dk 1, Yanga wanaanza kwa kufanya shambulizi na kupata kona ambayo inachongwa lakini JKT wanaokoa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni