pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumapili, 23 Oktoba 2016
Atimae: Babi ruksa kukipiga ligi kuu Zanzibar
Baada ya klabu ya Jang’ombe kushindwa kumtumia kiungo mshambuliaji wao Abdi Kassim ‘Babi’ kwenye michezo yake minne iliyopita, hatimaye klabu hiyo itaweza kumtumia mchezaji huyo.
Imani ya Jang’ombe kumtumia Babi kwenye michezo yake ya ligi kuu Zanzibar inakuja kufatia Shirikisho la soka Ulimwenguni FIFA, kuwasilisha kibali cha mchezaji huyo – ITC kwa Chama cha Mpira wa miguu Zanzibar.
Kibali hicho kilichoombwa mapema mwezi huu kilichelewa kuwasilishwa na kupelekea mchezaji huyo kushindwa kuonekana uwanjani wakati timu yake ilipokua inapambana.
Kupatikana kwa kibali hicho cha Kimataifa kumewafanya mashabiki wa timu hiyo kushusha presha kwani wanaimani kubwa kuwepo kwa Babi uwanjani kutaisaidia timu yao kulamba alama tatu kwa wapinzani wao.
Abdi Kassim alilazimika kutafutiwa kibali hicho kutoa FIFA kutokana na kumalizia msimu wake wa ligi nchini Malaysia akiwa na klabu ya UiTM.
Bila shaka mashabiki wa Taifa Jang’ombe na wapenda soka wa Zanzibar wataanza kumuona mchezaji huyo kesho (Jumatatu) saa moja usiku wakati timu yake itakapochuana na klabu ya Mafunzo ikiwa ni mwendelezo wa ligi kuu ya soka Zanzibar.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni