Jumapili, 30 Oktoba 2016

LIVE KUTOKA UWANJA WA UHURU; YANGA 3 VS 0 MBAO FC (KIPINDI CHA PILI)

Dk 78 sasa, kwa hali ilivyo, Mbao wanaonekana kupoteana kabisa, Yanga wanapiga pasi wanavyotaka. Lazima Mbao FC waimarishe uchezaji wao kwenye kiungo, la sivyo Yanga wanaweza kushindilia bao la nne GOOOOOOOOO Dk 75, Tambwe anaifungia Yanga bao safi kabisa akiunganisha pasi safi ya Simon Msuva DK 74, Donald Ngoma anaruka na kupiga kichwa mpira wa kurusha wa Twite, lakini safari hii kipa yuko makini SUB Dk 71, Yanga wanamtoa Chirwa na nafasi yake inachukuliwa na Donald Ngoma KADI Dk 70 Ndikumana analambwa kadi ya njano kwa kumkwatua Haji Mwinyi SUB Dk 64, Yanga wanamtoa Hassan Kessy na nafasi yake inachukulwia na Thabani Kamusoko, maana yake Mbuyu Twite anakwenda pembeni kulia Dk 62, Tambwe anaachia kombora hapa linagonga mwamba na kutoka nje, ilikuwa ni al manusura SUB Dk 56, Juma Mahadhi anaingia kuchukua nafasi ya Kaseke GOOOOOOOOOO Dk 55, mpira wa kurusha wa Twite unakwenda moja kwa moja kwa moja wavuni kipa kuupangulia ndani SUB Dk 54 Venance Ludovic anaingia Damas Msiba kwa upande wa Mbao FC Dk 50, Yanga wanazidi kusukuma mashambulizi, Niyonzima anaangushwa hapa, anatibiwa GOOOOOOOOO Dk 49, Bossou anafunga bao lakini mpira unagusa mkono wake kabla ya kuingia wavuni. Ilikuwa ni baada ya kuunganisha krosi ya Niyonzima aliyepiga mpira wa adhabu Dk 46, Yanga wanaanza kwa kasi wakishambulia zaidi na wanaonekana wanataka bao la mapema MAPUMZIKO DAKIKA 2 ZA NYONGEZA Dk 44, Tambwe anapokea pasi nzuri ya Niyonzima na kupiga vizuri lakini mpira unatoka kiduchu kabisa SUB Dk 42, Salum Sued anakwenda nje kwa upande wa Mbao FC, nafasi yake inachukuliwa na Maganga Dk 37, Bado hakuna hata shambulizi kubwa. Inaonekana wazi Yanga wanahitaji mtu wa kulazimisha kama Ngoma vile. Chirwa na Tambwe wanaonekana 'kutoiva' pamoja Dk 30, bado inaonekana hakuna shambulizi kali zaid ya kona. Dk 24, Mbao wanapata kona baada ya Bossou kulazimika kutoa nje mpira, inachongwa lakini Dida anadaka vizuri kabisa Dk 18, Yanga inapata kona ya kwanza baada ya beki Mbao kumuwahi Msuva na kuutoa. Inachongwa lakini haina manufaa Dk 14, hakuna shambulizi kali kwa upande wowote, inaonekana kila upande bado haujajipanga katika umaliziaji Dk 8, Chirwa anapiga shuti kimo cha nyoka lakini linatoka sentimeta chache kabisa nje ya lango la Mbao Dk 6, krosi safi ya Kaseke, Msuva anaunganisha vizuri kabisa lakini anashindwa kulenga lango. Yanga imetumia takribani dakika nne ikigongena vizuri kabisa Dk 1 mpira unaanza taratibuuu kila upande unaonekana ukiwa makini kwa kutaka kufunga na kuepuka kufungwa

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni