Jumatano, 26 Oktoba 2016

LIVE KUTOKA UHURU: YANGA 2-0 JKT RUVU (KIPINDI CHA PILI)

GOOOOOOO Dk 61, Tambwe anafunga bao safi kabisa akiwa ametulia baada ya mabeki wa JKT kumsahau KADI Dk 61, Nashon Naftal analambwa kadi ya njano kwa kumrukia Mwinyi SUB Dk 60, Michael Aidan anaingia kuchukua nafasi ya Kindamba ambaye ameumia baada ya kugongwa na Mwinyi wa Yanga Dk 59, Kindamba anatolewa nje baada ya kufanyiwa huduma ya kwanza, inaonekana amechanika kichwani KADI Dk 57, Mwinyi analambwa kadi ya njano baada ya kumgonga kichwani mchezaji wa JKT, Omary Kindamba anayetibiwa SUB Dk 56, Yanga wanafanya mabadiliko yao ya kwanza, wanamtoa Ngoma na nafasi yake inachukuliwa na Amissi Tambwe Dk 54, Yanga wanagongeana vizuri, Haji Mwinyi anapiga krosi matata kabisa lakini Msuva anaunganishwa kwa kichwa cha mwendokasi Dk 52, Chirwa tena, akiwa hatua tatu kutoka alipo kipa wa JKT lakini anashindwa kuunganisha mpira Dk 46 kipindi cha pili kimeanza, Yanga wakiwa wanapeleka mashambulizi yao Kusini na JKT wanasukuma Kaskazini MAPUMZIKO DAKIKA 3 ZA NYONGEZA Dk 45, JKT wanapata kona lakini haina mafanikio Dk 44 Yanga wanapoteza wanapotez anafasi nyingine tena ya wazi hapa baada ya Msuva kuukosa mpira KADI Dk 39 kadi ya kwanza katika mchezo huu inatoka, Kassim Kisengo wa JKT anazawadiwa baada ya kumuangusha Chirwa Dk 37, nafasi nyingine kwa Yanga, Ngoma akiwa hatua tano na kipa, anapiga kichwa pembeni juuuuuu Dk 35, krosi safi ya Kessy, Ngoma anabaki na kipa, anampa mikononi Dk 34 Chirwa anawahadaa mabeki wa JKT, anapiga shuti safi kabisa, lakini kipa anapangua na mabeki wanaosha Dk 30, yuko chini anatibiwa baada ya kugongwa na beki wa JKT wakati akiokoa mpira, anatoka nje na baadaye mwamuzi anamruhusu kuendelea na mchezo Dk 29, Kessy anaachia shuti kali tena, lakini mpira unawababatiza mabeki wa JKT na kuokoa Dk 27 sasa, Yanga ndiyo wanaonekana kumiliki zaidi mpira katikati ya uwanja lakini hakuna shambulizi kubwa hata moja Dk 22, Atupele anampa Dilunga pasi safi kabisa lakini shuti lake, mpira unatoka sentimeta chache nje ya lango la JKT Dk 19, Kessy anapiga mpira unakwenda moja kwa moja na kugonga mwamba wa juu, mabeki JKT wanaokoa Dk 12, Kamusoko naye anashindwa kuukwamisha mpira wavuni akiwa amebaki na kipa. Yanga wanazichezea hizi nafasi na wanapaswa wawe makini sana Dk 11, Yanga wanafanya shambulizi jingine, mpira unamfikia Chirwa akiwa na kipa peke yake, lakini anampa mikononi Dk 10, Kaseke anawahadaa mabeki JKT na kutoa pasi safi kwa Msuva lakini anapiga shuti kuuubwaaaa Dk 8, JKT wanachonga kona yao ya pili lakini mpira unaokolewa mbali kabisa na Yondani Dk 7, Atupele Green anaingia vizuri na kuachia shuti kali, Yondani anazuia na kuwa kona, inapigwa inakuwa nje tena, kona GOOOOOO DK 6 Chirwa anaifungia Yanga bao kwa shuti kali baada ya beki wa JKT kuanguka na kuuacha mpira nyuma, MSuva akauwahi na kumpa Chirwa ambaye amemaliza kazi Dk 1, Yanga wanaanza kwa kufanya shambulizi na kupata kona ambayo inachongwa lakini JKT wanaokoa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni