Jumanne, 25 Oktoba 2016

Tamko la Zesco United baada ya taarifa za kocha wao katua Yanga

Klabu ya Zesco United imekuja juu baada ya kusikia kocha wake George Lwandamina yupo Tanzania akifanya mazunguzo ya kukamilisha taratibu za kujiunga na klabu ya Yanga huku taarifa nyingine zikidai tayari kocha huyo ameshamwaga wino wa kuifundisha Yanga kwa miaka miwili. Inaelezwa Lwandamina alitua Dar October 23 kukamilisha taratibu za kuchukua nafasi ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo Hans van der Pluijm ambaye ameshajiuzulu baada ya kusikia ujio wa Lwandamina. Uongozi wa Yanga bado haujatangaza rasmi kama umeshaingia mkataba na kocha huyo raia wa Zambia lakini kwa upande wa Lwandamina yeye amekuwa akisisitiza uwepo wake nchini ni kwa sababu zake za kibiashara. Klabu ya Zesco United kupitia ukurasa wake rasmi wa facebook, imetoa taarifa kwa vyombo vya habari ikidai imepokea taarifa za vyombo vya habari kwamba kocha wao yupo Tanzania akifanya mazungumzo na klabu ya Yanga tofauti na alivyoomba ruhusa wakati anaondoka. Hii hapa taarifa ya Zesco United kuhusu kocha George Lwandamina… To∶ ALL MEDIA HOUSES From ∶ ZESCO UNITED FOOTBALL CLUB 25th October 25, 2016 RE∶ GEORGE LWANDAMINA Zesco United would like to acknowledge receiving Media reports suggesting that head Coach, George Lwandamina is in Tanzania having talks and at the verge of signing a two year contract with Young Africans Sporting Club. Lwandamina has a three year running contract that expires in January 2017 and the club has not entered into negotiations to have the contract extended and Lwandamina has not communicated his intentions at the end of the contract. As far as the Club is concerned, Lwandamina is in Monze attending a family bereavement as he stated on Sunday when he sought permission to leave from the Team Manager, Mr Mabvuto Banda and is expected to return to camp today for the midweek rescheduled game against Nkwazi FC in Lusaka tomorrow. Zesco United would like to state that if indeed these media reports are true, Lwandamina will be in breach of his contract with the club, we believe he is a professional and is expected to behave as such. We believe that he is aware of his contractual obligations and implications of a possible breach. Issued by Richard Mulenga (Mr) and Katebe Chengo (Ms) Acting General Secretary and Media Officer Tafrisi isiyo rasmi Zesco United imepokea taarifa kutoka vyombo vya habari zinazodai kwamba, kocha wao mkuu George Lwandamina yupo Tanzania akifanya mazungumzo huku taarifa nyingine zikisema tayari amesaini mkataba wa miaka miwili na klabu ya Yanga SC. Lwandamina anamkataba wa miaka mitatu unaomalizika January 2017, klabu bado haijafanya makubaliano yoyote huku Lwandamina akiwa hajawasiliana na uongozi kueleza malengo yake baada ya mkataba kumalizika. Hadi sasa uongozi unatambua kwamba, Lwandamina yupo nyumbani kwao Monze kuhudhuria matanga kama alivyoomba ruhusa siku ya Jumapili kwa Team Manager, Mr Mabvuto Banda na anatarajiwa kurejea kambini leo kwa ajili ya mchezo wa katikati ya wiki dhidi ya Nkwazi FC utakaopigwa kesho huko Lusaka. Endapo taarifa hizo za vyombo vya habari zinaukweli, Lwandamina atakuwa anakwenda kinyume na mkataba wake na Zesco United, tunaamini yeye ni mweledi na tunatarajia ataishi hivyo. Tunaamini anatambua makubaliano yaliyopo kwenye mkataba wake na hatua zitakazochukuliwa kutokana na kwenda kinyume na mkataba. Chanzo: https://www.facebook.com/ZescoUnitedFc/

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni