Dk 12, Kamusoko naye anashindwa kuukwamisha mpira wavuni akiwa amebaki na kipa. Yanga wanazichezea hizi nafasi na wanapaswa wawe makini sana
Dk 11, Yanga wanafanya shambulizi jingine, mpira unamfikia Chirwa akiwa na kipa peke yake, lakini anampa mikononi
Dk 10, Kaseke anawahadaa mabeki JKT na kutoa pasi safi kwa Msuva lakini anapiga shuti kuuubwaaaa
Dk 8, JKT wanachonga kona yao ya pili lakini mpira unaokolewa mbali kabisa na Yondani
Dk 7, Atupele Green anaingia vizuri na kuachia shuti kali, Yondani anazuia na kuwa kona, inapigwa inakuwa nje tena, kona
GOOOOOO DK 6 Chirwa anaifungia Yanga bao kwa shuti kali baada ya beki wa JKT kuanguka na kuuacha mpira nyuma, MSuva akauwahi na kumpa Chirwa ambaye amemaliza kazi
Dk 1, Yanga wanaanza kwa kufanya shambulizi na kupata kona ambayo inachongwa lakini JKT wanaokoa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni