Jumatatu, 24 Oktoba 2016

Mrithi wa Pluijm asaini miaka miwili Yanga

Taarifa inayosambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii ni ujio wa kocha mpya George Lwandamina anayetajwa kuchukua nafasi ya Babu Hans van der Pluijm kwenye kikosi cha Yanga SC. Jana iliripotiwa kocha huyo ameshatua jijini Dar kwa ajili ya kumaliza taratibu za kukabidhiwa mikoba kutoka kwa Mholanzi Van Pluijm, lakini taarifa iliyopo sasa ni kwamba, Lwandamina tayari amesaini mkataba wa miaka miwili kuifundisha klabu ya Yanga. Awali ilielezwa kuwa, baada ya kocha huyo mzambia kupewa majukumu ya kukinoa kikosi cha Yanga, Pluijm atakuwa Mkurugenzi wa ufundi wa mabingwa hao watetezi wa taji la VPL. Taarifa zilizopo ni kwamba klabu ya Yanga itamleta Mkurugenzi wa ufundi kutoka nchini Ureno.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni