Wakati harakati za mabadiliko ya uendeshaji wa vilabu ikiwa ndiyo habari ya town, Baraza la michezo Tanzania BMT limezitaka klabu za Simba na Yanga kusitisha mara moja mchakato wa mfumo wa mabadiliko wa uendeshaji wa klabu mpaka watakapokubaliana na wanachama wao.
Akitangaza taarifa hiyo mbele ya waandishi wa habari, Katibu Mkuu wa BMT Mohamed Kiganja amesema kama Serikali, inapenda klabu hizo zifanye mabadiliko ya kimfumo lakini zifuate utaratibu.
Kiganja amevitaka vlabu vyote viwili kufanya makubaliano na wanachama wao kwa amani kabla ya kufanya mabadiliko hayo.
Serikali imesema imesitisha zoezi hilo hadi pale taratibu nyingine zitakapofuatwa baada ya kuona zoezi zima limekiuka taratibu.
Serikali imevitaka vilabu vya Simba na Yanga ziachwe kwanza kwa wanachama wao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni