Jumamosi, 29 Oktoba 2016

Arsenal kileleni baada ya Giroud na Sanchez kuitikisa Sunderland.

Klabu ya Arsenal imekwea hadi nafasi ya kwanza kwenye ligi ya England baada ya kupata ushindi wa mechi yake ya saba kwa kuilaza Sunderland 4-1 ugani Light. Alexis aliipa gunners bao la uongozi katika dakika ya 19 baada ya kuandaliwa pasi na Alex Oxlade Chamberlain. Hata hivyo uongozi huo ulidumu hadi dakika ya 65 baada ya Defoe kuipa Sunderland bao la kusawazisha kupitia mkwaju wa penalti. Petr Cech alimtega mshambulizi Duncan Watmore na kupewa kadi ya njano. Dakika chache baadaye, Wenger alifanya mabadiliko uliomwezesha Giroud kuchukua nafasi ya Alex Iwobi aliyeonekana kuwa na kazi ngumu dhidi ya mabeki wa Sunderland. Arsenal alichukua uongozi kunako dakika ya 71 baada ya nguvu mpya Oliver Giroud kuunganisha pasi ya beki Kieran Gibbs,kwenye wavu. Gibbs alichukua nafasi ya Nacho Monreal anayeuguza majeraha.  Ushambulizi wa Sunderland ulitishia uongozi wa Arsenal, lakini Giroud aliipa Arsenal matumaini ya kuondoka na alama tatu katika dakika ya 76 baada ya kufunga kupitia krosi ya Kona iliyiochanjwa na kiungo Mesut Ozil. Dakika mbili baadaye Alexis Sanchez alizidisha uchungu kwa mashabiki wa Sunderland walioonekana kuondoka uwanjani kwa kupachika bao la nne. Sanchez alimtesa kipa Jordan Pickford baada ya Ramsey kumuandalia pasi. Bahati ya beki Kieran Gibbs haikutimia baada ya mkwaju wake kugonga lango, lakini Sanchez alifunga kazi na kuihakikishia Arsenal ushini huo muhimu. Arsenal inaongoza ligi ikiwa na alama 23 ingawa klabu za Machester City na Liverpool bado hazicheza. Ushindi huo umeipa Arsenal motisha huku ikisubiri kuialika Tottenham Hotspurs uwanjani Arsenal wikendi ijayo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni