Jumanne, 25 Oktoba 2016

Magoli ya Sturridge yaipa ushindi Liverpool dhidi ya Tottenham EFL Cup

Liverpool imeichapa Spurs 2-1 katika mchezo wa EFL Cup na kufuzu raundi inayofuata kuendelea kuwania taji hilo. Wawili hao walikutana White Hart Lane mapema mwanzoni mwa msimu huu na kushuhudia mchezo huo ukimalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1. Usiku wa October 25 Liverpool ikiwa kwenye ubora wake iliibuka na ushindi wa magoli 2-1 na huenda ‘majogoo wa jiji’ wangepata ushindi zaidi ya huo. Daniel Sturridge alikuwa shujaa wa mchezo huo baada ya kufunga magoli yote mawili katika mchezo huo. Licha kuwa Sturridge hakuwa kwenye kiwango bora atika siku za hivi karibuni, magoli yake hayajaja kama surprise kutokana na nyota huyo kufunga magoli 10 katika mechi 8 zilizopita kwenye michuano hiyo. Ameshindwa kufunga katika mechi 7 zilizopita kabla ya mchezo dhidi ya Spurs ukame wa magoli wa muda mrefu tangu alipojiunga na Liverpool, lakini amekuwa akiingia na kutoka kwenye timu kutokana na kusumbuliwa na majeraha. Baada ya kupewa nafasi ya kuongoza safu ya ushambuliaji, ameonesha ni kwa jinsi gani yupo vizuri na dakika za mwisho alikaribia kufunga goli ambalo lingemfanya afunge hat-trick ya kwanza akiwa na klabu ya Liverpool. Matokeo ya mechi zote za EFL October 25, 2016

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni