pata dondoo mbalimbali za michezo ya ndani na nje ya nchi.mompondazy itakujuza kila kitu.
Jumapili, 23 Oktoba 2016
HABARI ZA KIDAKUZI: Kocha anayetajwa kuchukua nafasi ya Pluijm atua Dar
Kuna tetesi zimeenea kwenye mitandao ya jamii kwamba, George Lwandamina kocha wa klabu ya Zesco United ya nchini Zambia anayehusishwa na mpango wa kujiunga na Yanga tayari ameshawasili nchini.
Inadaiwa Lwandamina atakuchukua nafasi ya kocha wa sasa Hans Van Pluijm ambaye kwasasa ni kocha mkuu wa Yanga ambao ndio mabingwa watetezi wa taji la ligi kuu Tanzania.
Habari ambazo hazijathibitishwa na uongozi wa Yanga zinadai kuwa, endapo uongozi utaamua kulibadili benchi la ufundi, Van Pluijm atakuwa mkurugenzi wa ufundi wa Yanga.
Lwamdamina mwenye umri wa miaka 53 aliwahi kucheza nafasi ya ulinzi kwenye timu ya taifa ya Zambia lakini pia aliwika wakati akiichezea klabu ya Mufulira Wanderers.
Mwaka 2014 miamba ya Ndola ZESCO United ilimsajili George Lwandamina kuwa kocha mkuu wa timu hiyo. Katika msimu wake wa kwanza Lwandamina aliisaidia ZESCO kutwaa taji la ligi kisha kulitetea msimu uliofuta.
Kutwaa ubingwa wa ligi ya Zambia kulimfanya ashinde tuzo ya kocha bora wa mwaka wa ligi hiyo mara mbili mfululizo.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni