Jumamosi, 1 Oktoba 2016

LIVE KUTOKA TAIFA: GOLI LA MKONO LA TAMBWE LAZUA GUMZO YANGA 1 VS SIMBA 0 (KIPINDI CHA KWANZA)

Dk 45, Mavugo anaingia vizuri, anamtola Juma Abdul na kupiga shuti, BArthez anaokoa na kuwa kona Dk 44, Yanga wanashambulia tena shuti hapa la Mahadhi lakini linakuwa dhaifu Dk 43, Mavugo anajaribu shuti lakini linatoka nje sentimeta chache Dk 42, Tambwe yuko chini pale baada ya kuangushwa na mwamuzi anaonya pale Dk 40, Kichuya anaingia vizuri kabisa anaachia shuti kali lakini halikulenga lango Dk 37, Ngoma anawachambua mabeki wa Simba kama karanga hapa na kuachia shuti kali kabisa, lakini Angbani anadaka vizuri Dk 30 hadi 35, mpira unachezwa zaidi katikati ya uwanja hata hivyo Simba wanaonekana hawajatulia baada ya kulalamikia lile bao la Tambwe ambaye alishika na kulalamikiwa na wachezaji hao Dk 29, mpira bado umesimama, mashabiki wa Simba wanang'oa viti, polisi wanapiga mabomu ya machozi KADI Dk 28 Mwamuzi anamlamba kadi nyekundu nahodha wa Simba Jonas Mkude, haijajulikana kama alifanya nini Dk 27, walinzi wanalazimika kuingia uwanjani kuwapoeza wachezaji wa Simba wakilalamika kama wanasusia baada ya Tambwe kufunga bao hilo wakisema alishika GOOOOOOOOOOOO Dk 26, Tambwe anaipatia Yanga bao safi baada ya kugeuka na mpira ukiwa mkononi mbele ya Lufunga na kufunga kirahisi kabisa Dk 24, Mpira wa kurushwa, Ajibu anaunganidha shuti juujuu hapa lakini anashindwa kulenga lango na mashabiki wa Yanga wanazomeee buuuuuu Dk 23, Kichuya anaangushwa hapa, mwamuzi anasema faulo lakini yeye analalmika huku upande mwingine Bossou naye akiwa analalamika kwamba amepigwa kiwiko Dk 22, Ajibu anajaribu kuwachambua mabeki wa Yanga, anaanguka lakini mwamuzi anamwambia amka twende kazini baba Dk 20, Simba wanagomngeana vizuri zaidi lakini wanakuwa si wazuri katika kumalizia Dk 16, Yanga wanaonekana kutulia zaidi na kucheza soka safi zaidi huku Simba wakihaha kuwakapa Dk 14, Krosi nzuri ya Juma Abdul, Kamusoko anapiga kichwa kinatoka sentimeta chache nje juu ya lango la Simba Dk 11, Mavugo anawekwa chini na Yondani, anatibiwa na kutolewa nje. Mpira unaendelea Dk 9, mpira wa faulo wa Mavugo, unababatiza ukuta wa mabeki wa Yanga na kuokolewa Dk 7, Zimbwe anatelekeza lakini anauwahi mpira na kuutoa, inakuwa kona,inachongwa hatari hapaa, shuti la Tambwe linatoka sentimeta chache kabisa Dk 6, Kichuya anatoa pasi nzuri kwa Ajib, anageuka na kupiga, mpira unaingia langoni. Lakini mwamuzi Saanya anasema ilikuwa offside tayari DK 3, Kazimoto anaangushwa wakati akienda kufunga, mwamuzi anasema faulo, anaipiga Ajibu lakini juuuuu Dk 1, mechi imeanza taratibu na Yanga wanakuwa wa kwanza kufika kwenye lango la Simba.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni