Jumatatu, 31 Oktoba 2016

Beki wa klabu ya Barcelona Marlon Santos, ameshindwa kusafiri na timu hiyo kuelekea mjiu Manchester kufuatia kusahau pasi ya kusafiria (Passport). . Beki huyo wa kati ambaye kesho anaweza kucheza mechi yake ya kwanza ya UCL kufuatia kuumia kwa Gerard Pique, ameonekana kujawa na furaha mpaka kusababisha kusahau Passport nyumbani. Hata hivyo klabu ya Barcelona imeripoti kuwa beki huyo atapanda ndege za kawaida leo kutoka uwanja wa ndege wa El Prat na kujiunga na kikosi jijini Manchester Marlon,21, ambaye amejiunga na Barca B kwa mkopo kutokea Fluminense msimu huu , baada ya kuonesha uwezo mzuri katika mechi za maandalizi ya msimu, sasa ameitwa katika kikosi cha kwanza kufuatia baadhi ya wachezaji kuwa majeruhi.

THOMAS MASHALI SASA KUZIKWA KESHO JUMATANO

Mazishi ya bondia Thomas Mashali aliyeuwawa yanatarajia kufanyika kesho jijini Dar es Salaam. Baba mzazi wa Mashali amesema wameamua kufanya mazishi hayo Jumatano kwa kuwa wanapisha uchunguzi wa polisi. “Tumewaachia kidogo polisi wamalizie kazi yao, lakini mazishi yatakuwa Jumatano badala ya Jumanne kama ilivyokuwa hapo,” alisema. Msiba wa bondia huyo ambaye ameuwawa na watu wasiojulikana uko kwao Tandale jijini Dar es Salaam.

YANGA YATUA MBEYA TAYARI KWA AJILI YA MECHI DHIDI YA CITY, MASHABIKI WAWAPA MAPOKEZI YA HESHIMA

Yanga wametua mjini Mbeya wakiwa tayari kwa ajili ya mechi yao ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbeya City, keshokutwa. Mashabiki na wanachama wa Yanga walijitokeza kwenye Uwanja wa ndege mjini humo kuwapokea vijana wao huku wakiwaonyesha heshima kubwa.  Yanga inatarajia kufanya mazoezi leo chini ya Kocha Hans van Der Pluijm ili kufanya maandalizi ya mwisho kabla ya mechi hiyo ya Jumatano.

MASHALI AMEUWAWA SIKU CHACHE BAADA YA KUBADILI DINI NA KUWA MWISLAMU, ALIKUWA AKIITWA MOHAMMED

Wapenda ngumi nchini wako katika majonzi makubwa baada ya kifo cha bondia nyota, Thomas Mashali. Mashali ameuwawa katika moja ya viunga vya jiji la Dar es Salaam, ikielezwa aliokotwa eneo la Kimara ingawa kuna wengine wanasema ameokotwa eneo la Tabata. Kitu ambacho Watanzania wengi hawakukijua ni kwamba, wakati mauti yanamkuta, Mashali alikuwa amebadili dini siku chache, kutokuwa kuwa Mkristo hadi Mwislamu, akaamua kuacha kutumia jina la Thomas na alikuwa akitumia jina la Mohammed. Katibu Mkuu wa Shirikisho la Ngumi za Kulipwa (PST), Anthony Rutta amesema, Mashali kweli alibadili dini. "Kweli alikuwa anaitwa Mohammed, hili alitueleza mwenyewe kwamba aliamua mwenye kwa hiari yake kuwa mwislamu," alisema Rutta.

Mchambuzi wa soka BBC na mshambuliaji wa zamani wa England & Newcastle mwenye rekodi ya kuwa mfungaji bora wa EPL wa wakati wote - Alan Shearer amesema kwamba Sergio Kun Aguero ndio mchezaji pekee wa kiwango cha dunia wa EPL ambaye anaweza kuingia kwenye first eleven ya timu yoyote duniani. Nini maoni yako kuhusiana na hili, unadhani Aguero pekee ndio mwenye sifa hizo??? Karibu tujadili pamoja.

Mkataba mpya wa Gareth Bale na Real Madrid. Kwa mwaka atakuwa akilipwa shilingi billioni 95,148,000,000 Kwa mwezi billioni 7,929,000,000 Kwa wiki atalipwa 1,982,250,000 Kwa siku ataingiza 283,176,306 Kwa saa 1 ataingiza 11,798,352 Kwa dakika 1 ataingiza 195,582 Mkataba huu unamfanya Bale kuwa mwanasoka anayelipwa fedha nyingi zaidi. *Malipo haya kabla ya kukatwa kodi*

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger asema mwezi November utaamua uelekeo wa kikosi chake msimu huu kwenye Primier League

CHEKA AMLILIA MASHALI, KUMBUKA ALIMPIGA MARA YA MWISHO WALIPOKUTANA

Bondia mahiri nchini, Francis Cheka ameonyesha hisia zake kutokana na kifo cha bondia mwingine, Thomas Mashali. Mashali ameuwawa na watu wasiojulikana, inadaiwa mwili wake umetupwa katika eneo la Kimara jiji Dar es Salaam. Kupitia mtandao wa facebook, Cheka ameandika akionyesha masikitiko yake kwa Mashali ambaye walipokutana mara ya mwisho, Mashali alimshinda Cheka na kuwa bondia namba moja nchini, kwani pia alikuwa amewahi kumshinda Dulla Mbabe ambaye sasa anatamba. Cheka ameandika: “Ilikuwa ni heshima kuingia ulingo mmoja na wewe ndugu yangu Thomas Mashali, tulipanga tukutane tena 26/11, kweli hakuna aijuae kesho, oila Mungu. “Ulale mahali pema peponi ndugu yangu, Mungu akutangulie.” Yassin Abdallah ‘Ustaadhi’, mmoja wa viongozi wakongwe wa mchezo wa ngumi amethibitisha na kusema mwili wa Mashali upo kwenye chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Dondoo muhimu: EPL Weekend iliyopita

Na Athumani Adam Ligi kuu nchini England iliendelea siku ya Jumamosi na Jumapili kwa michezo tisa kufanyika kwenye viwanja mbali mbali. Baada ya kumalizika kwa mechi hizo za mzunguko wa kumi zipo rekodi mbali mbali ambazo zilitokana matokeo ya mechi hizo Makala hii inakusimulia takwimu muhimu ambazo ziliandikwa baada ya kumalizika kwa michezo hiyo ya wikiendi October 30 na 31. Namba 1 (Ander Herrera) Kwenye mchezo dhidi ya Burnley kiungo wa Man United, Herrera alipata kadi nyekundu kwenye dakika ya 68 ya mchezo. Kadi ambayo Herrera alioneshwa na mwamuzi Mark Clatternburg siku ya Jumamosi inakuwa kadi nyekundu ya kwanza ya Herrera kwenye ligi kuu nchini Uingereza. Mara ya mwisho kwa mchezaji wa Man Utd kuoneshwa kadi nyekundu kwenye uwanja wa Old Trafford ilikuwa mwaka 2014 ambapo nahodha Wayne Rooney alipata kadi kwenye mchezo dhidi ya Westbrom Namba 2 (Sunderland, Jack Wilshere) Klabu ya Sunderland ambayo ipo chini ya kocha David Moyes imekuwa timu ya kwanza kuwa na pointi chache zaidi ligi kuu England baada ya kucheza kucheza mechi kumi. Sunderland hadi sasa ina pointi mbili wikiendi walipoteza mchezo dhidi ya Arsenal kwa 1-4. Mara ya mwisho kushuhudia timu kuwa na pointi kama za Sunderland ilikuwa msimu wa 1995/96 kwa timu ya Man City. Pia Kiungo wa Arsenal aliye kwa mkopo kwenye klabu ya Bournemouth, Jack Wilshere alifanikiwa kucheza mechi ya pili kwa dakika zote tisini wikiendi hii. Bournemouth walipoteza dhidi ya Middlesbrough kwa mabao 2-0. Namba 3 (Vicent Janssen) Mshambuliaji wa Tottenham Hotspurs, Vicent Janssen aliifungia timu yake bao la kuongoza dakika ya 44 kwenye mchezo dhidi ya Leicester. Bao la Janssen linamfanya kuwa na mabao matatu kwenye klabu ya Spurs huku mabao yote akiwa amefunga kwa njia ya penati. Mara ya mwisho kwa Wlishere kucheza dakika tisini ilikuwa ni mwezi September 2014. Namba 4 (Chelsea) Kwenye mechi tano za karibuni, Klabu ya Chelsea inaonekana kuwa na safu bora ya ulinzi baada ya kupata Clean Sheet 4 (kucheza bila kuruhusu bao). Clean Sheet ya nne ya hivi karibuni ilikuwa siku ya Jumapili ambapo Chelsea ilipata ushindi wa 2-0 dhidi ya Southampton. Namba 6 (Zlatan Ibrahimovic) Ukame wa mabao umeendelea kwa mshambuliaji wa Man United Zlatan Ibrahimovic. Zimepita mechi sita tangu Ibrahimovic alipofunga mara ya mwisho kwenye mchezo dhidi ya mahasimu wao wa jiji la Manchester, Man City mwezi September mwaka huu. Mara ya mwisho kushudia Zlatan kucheza mechi sita za ligi bila kufunga ilikuwa December mwaka 2007 alipokuwa kwenye klabu ya Inter Milan ya Italia. Man Utd ilitoka suluhu dhidi ya Burnley nyumbani, huku mlinda malango wa Burney aliibuka shujaa kwa kuokoa mashuti kumi na moja. Namba 10 (Tottenham Hotspurs, Westbrom) Sare ya 1-1 dhidi ya mabingwa wa msimu uliopita Leicester City umeifanya timu ya Tottenham Hotspurs kucheza mechi kumi bila ya kufungwa. Mara ya mwisho kwa Spurs kufanya hivyo ikiuwa ni msimu wa 1990/91. Hadi sasa Spurs wamecheza mechi kumi, kushinda mechi tano na kutoka sare mara tano. (w5 D5, L0) matokeo ambayo yanaifanya Spurs kuwa timu pekee ambayo hajipoteza mchezo msimu huu. Klabu ya Westbrom imepoteza michezo yote kumi ya hivi karibuni ambayo timu hiyo imecheza dhidi ya Man City. Wikiendi iliyopita Westbrom waliwa nyumbani walifungwa na Man City 4-0

KIFO CHA MASHALI CHAGUBIKWA NA RUNDO LA TAARIFA TATA

Kifo cha bondia maarufu nchini, Thomas Mashali kimetawaliwa na utata mkubwa, kila mmoja akisema lake. Mashali ameokotwa akiwa amefariki dunia baada ya kuwawa na watu wasiojulikana, lakini hakuna mwenye uhakika ilikuwaje. Pamoja na hivyo, kumekuwa na taarifa kwamba alikuwa na wenzake, walikwenda kuvamia sehemu kwa ajili ya kuiba kwenye duka la Tigo Pesa. Taarifa nyingine zinasema Mashali alikwenda kumdai mtu, wakapishana kauli na yule mtu akamuitia watu kuwa ni mwizi na taarifa nyingine zinaeleza kwamba Mashali aliuwawa na watu ambao alizozana nao wakati wakiburudika na kinywaji baa. Katibu Mkuu wa moja ya mashirikisho ya ngumi za kulipwa nchini la PST, Anthony Rutta amekiri wao kupokea taarifa hizo. "Ni kweli kuna taarifa zinachanganya sana kama hiyo sijui walikwenda kuiba kwenye Tigo Pesa, wengine wanasema aliitiwa mwizi na mtu anayemdai pia kuna ishu inasema kwamba aligombana na vijana wa Kichaga, wakamshambulia. "Sasa haijajulikana, tumeamua tuliachie jeshi la polisi lifanye kazi yake. Kama kuna tatizo kwa marehemu au wengine, tutajua," alisema Rutta. Taarifa za kifo cha Mashali zinaonekana kuwashitua watu wengi ambao walikuwa wanaujua ubora wake na inaelezwa jana alikuwa katika kikao cha mabondia na alieleza machungu yake kuhusiana na mambo mengi ambayo hayakumfurahisha.

ULISHANGAA AJIBU KUWEKWA BENCHI, UFAFANUZI WA BENCHI LA UFUNDI LA SIMBA, HUU HAPA

Kocha Msaidizi wa Simba, Mganda, Jackson Mayanja, amesema mpaka sasa hakuna mchezaji ambaye amejihakikishia namba kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo, ndiyo maana staa wao Ibrahim Ajib amejikuta akipoteza nafasi mbele ya Mohammed Ibrahim ‘Cabaye’ kwenye michezo miwili mfululizo. Ajibu, licha ya kuwa na uwezo mkubwa lakini alilazimika kukaa benchi kwenye mechi za Toto Africans na Mwadui ambazo hata hivyo kikosi hicho kiliibuka na ushindi na kujikita kileleni kwa kujikusanyia pointi 32. Mayanja amesema kwamba lengo la kuweka suala hilo ni kutaka kuona kila mmoja anajituma kuhakikisha timu hiyo haina makundi kwa tabaka moja la wachezaji kujiona muhimu kuliko wenzao. “Kwetu hakuna mchezaji aliye staa kuliko mwenzake na hakuna mchezaji mwenye namba ndani ya kikosi cha kwanza kwani kila mmoja anaweza kukaa benchi na aliyekaa benchi akaanza, hiyo ni kulingana na mechi itakavyokuwa. “Tunafanya hivyo kwa ajili ya kutotaka kuwafanya kundi la wachezaji fulani kujiona muhimu ndani ya timu lakini pia hata watakapokosekana tuwe na uhakika kwamba tunavuna pointi tatu bila ya wasiwasi wowote ule. “Na siyo Ajibu peke yake ambaye amekutana na suala hili, bali tuna uwezo wa kumpumzisha yeyote yule na utaona ilimtokea Mavugo hivi karibuni na itaendelea kwa kila nafasi kwa ajili ya kuwafanya wachezaji kutobweteka na kuridhika kwani ikitokea hivyo basi tunaweza kupoteza ubingwa ambao tunausaka kwa kila hali,” alisema Mayanja. Hata hivyo, kwa mtazamo wa kawaida kuna wachezaji ambao hadi sasa katika kikosi cha Simba wameishajihakikishia namba katika kikosi hicho. Mfano mabeki Mohamed Zimbwe, Janvier Bukungu, Method Mwanjale, nahodha Jonas Mkude, viungo Muzamiru Yassin, kiungo Shiza Kichuya na kipa Vicent Agnban, hawa wanaonekana wamejihakikishia nafasi na wamekuwa wakiendelea kufanya vizuri ili kujihakikishia vizuri. SOURCE: CHAMPIONI

SIMBA, YANGA ZAKUTANA LAKINI ZASHINDWA KUSULUHISHA SUALA LA KESSY, MJUMBE CAF ATOA MWISHO ALHAMISI

Simba na Yanga, zimekutakana juzi Jumamosi lakini hazijafikia mwafaka kuhusiana na suala la beki Hassan Kessy ambaye Simba inamtuhumu kusaini kuichezea Yanga huku akiwa bado ana mkataba na Msimbazi. Mjumbe wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ambaye pia ni Mjumbe wa Heshima wa Shirikisho la Soka Afrika (Caf), Said El Maamry, aliyepewa jukumu la kuzisuluhisha timu hizo baada ya viongozi wa Yanga na Simba kwa kushirikiana na wale wa Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya TFF, kumpendekeza kuwa msuluhishi wao, amesema kwamba kilichosababisha lisipatiwe ufumbuzi hiyo juzi ni kutofika kwa mjumbe muhimu wa Yanga. Alisema mjumbe huyo ni Wakili wa Yanga, Alex Mgongolwa ambaye alishindwa kufika katika mkutano huo kutokana na kuwa na matatizo ya kifamilia yaliyomfanya asafiri kwenda mkoani Iringa. “Tulikutana jana (juzi) kwa ajili ya kulipatia ufumbuzi suala hilo lakini bahati mbaya hatukuweza kufanya chochote baada ya viongozi wa upande wa Yanga kutotimia ambapo wakali wao, Alex Mgongolwa hakuweza kutokea kutokana na kuwa na matatizo ya kifamilia. “Alipata msiba hivyo akasafiri kwenda Iringa kwa ajili ya suala hilo ndipo viongozi wa Yanga waliofika katika mkutano huo wakaniomba tuahirishe mpaka hapo atakapokuwa amerudi. “Kutokana na hali hiyo ilibidi nikubali ombi hilo, hivyo tutakutana tena siku ya Alhamisi baada ya Mgongolwa kurudi kwani anatarajia kurudi Jumanne (kesho),” alisema El Maamry. Timu hizo mbili zipo katika mvutano mkubwa ambapo Simba inataka ilipwe na Yanga dola 600,000 (zaidi ya Sh bilioni tatu) kama fidia kwa kile kinachodaiwa kuwa ilimsainisha Kessy mkataba wa ajira wakati akiwa bado yupo na mkataba na klabu hiyo. Simba ambao walifika kwenye kikao hicho kwa ajili ya kulimaliza suala hilo, ndiyo walalamikaji kwamba Kessy alisaini mkataba na Yanga wakati bado akiwa na mkataba nao. Kamati ya TFF ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji tayari ilikaa na kufikia uamuzi lakini haiikuutangaza na badala yake ikataka pande hizo mbili kukutana na kulisuruhisha. Taarifa za ndani zinaeleza, Yanga imepigwa kumbo katika kesi hiyo kwa kuonekana ilimsainisha Kessy akiwa na mkataba lakini kamati hiyo imetoa nafasi hiyo ya kiungwana kama pande hizo mbili zinaweza kumalizana. Iwapo Yanga ambao ni walalamikiwa na Simba ambao ni walalamikaji watashindwana katika hilo, kamati hiyo itatangaza adhabu hiyo ambayo itakuwa na athari kubwa zaidi kwa Yanga.

Jumapili, 30 Oktoba 2016

BREAKING NEWS: BONDIA MASHALI AUWAWA, MWILI WAKE WAOKOTWA VICHAKANI DAR

Bondia maarufu wa ngumi za kulipwa nchini, Thomas Mashali, hatunaye. Taarifa zinaeleza ameuwawa kwa kupigwa risasi na mwili wake kuokotwa vichakani maeneo ya Kimara jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo. Yassin Abdallah maarufu kama Ustaadhi, mmoja wa viongozi wakongwe wa mchezo wa ngumi amethibitisha na kusema mwili wa Mashali upo kwenye chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam. "Tumethibitishiwa hizo taarifa za majonzi kabisa, mwili upo Muhimbili na msiba upo kwao Tandale," alisema Ustaadhi.

GARETH BALE AMWAGA WINO KUENDELEA KUKIPIGA REAL MADRID: Real Madrid imemsainisha mkataba mpya winga wake Gareth Bale na kumfanya aendelee kudumu klabuni hapo mpaka 2022. Bale mchezaji wa zamani wa Southampton alijiunga na klabu hiyo akitokea Tottenham Hotspur mwaka 2013. Tiyari ameisaidia Madrid kushinda vikombe vitano katika misimu mitatu ya nyuma ikiwemo ligi ya mabingwa Ulaya mara 2 huku akifunga magoli 62 katika michezo 135. Viungo wawili wa timu hiyo Luka Modric na Toni Kroos nao pia walisaini mikataba mipya mwezi huu. Mkataba wa Bale unatajwa kuwa wa Euro 600,000 kwa wiki huku baada ya makato ya kodi ikiwa Euro 350,000 #BBC

Masharti ya Kocha mzambia yaliyosababisha Yanga kumuomba Hans Van Pluijm arejee. 1. George Lwandamina alitaka mshahara wa milioni 40. 2. Yanga ilitakiwa ivunje mkataba na ZESCO USD 300,000 3. Alitaka aje na wasaidizi watatu kila mmoja alipwe USD 10000 per month. 5. Alitaka apewe miaka mitatu kuandaa timu ndio aulizwe ubingwa wa TZ. 6. Robo tatu ya wachezaji ni wazee aliomba fungu la kutosha asajili na asiingiliwe, 7. Mkataba wake usiwe chini ya miaka mitatu.

HATIMAYE MAVUGO ASHUSHA MIKONO CHINI, AKIRI MAMBO NI MAGUMU, AOMBA MUDA...

Mshambuliaji Laudit Mavugo raia wa Burundi, bado hajafikia kile kiwango ambacho Watanzania wengi wapenda soka hasa wale wa timu ya Simba walikuwa wakikitarajia. Hali hiyo imezua maswali mengi na wakati mwingine inamuonyesha yeye kupaniki akitaka kuwaonyesha anaweza. Lakini baadaye amekubali, kwamba anahitaji muda ili ikifika siku, ataonyesha alichonacho. Mavugo ambaye alisajiliwa Simba akitokea Vital’O ya kwao Burundi, mara ya mwisho kufunga bao ilikuwa ni Oktoba 23 dhidi ya Toto kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar lakini kabla ya hapo alikuwa amecheza mechi sita mfululizo bila kufunga bao lolote. Juzi Jumamosi kwenye mchezo dhidi ya Mwadui mjini hapa alishindwa tena kucheka na nyavu. Alipata nafasi kibao lakini alizipoteza kabla ya kocha Joseph Omog kumtoa katika dakika ya 42 kipindi cha kwanza. Baada ya mchezo huo, Mavugo ambaye alianza ligi kwa mbwembwe na kuonekana atakuwa supastaa wa Simba, alisema: “Hakika naomba mashabiki wa Simba wanipe muda kwani bado sijazoea baadhi ya viwanja vya hapa Tanzania, kwani kuna viwanja vizuri lakini pia vingine ni vibovu. “Kule kwetu Burundi hakuna viwanja vibovu kama huku Tanzania, ndiyo maana kule nilikuwa nafunga mabao mengi lakini huku napata tabu sana jinsi ya kufunga lakini nina imani kuwa nitayazoea mazingira na nitafanya vema.” Juzi, Mavugo ambaye msimu huu tayari ana mabao manne, alikosa mabao matatu ya wazi na kulazimika kutolewa nje mapema kabisa na nafasi yake ikachukuliwa na Ame Ally aliyeiimarisha safu ya ushambuliaji ya Simba huku akitoa pasi ya bao la tatu la klabu hiyo lililofungwa na Mohammed Ibrahim. Pamoja na papara, Mavugo amekuwa akionyesha ni mchezaji anayeweza kufanya vizuri zaidi ya alipofikia lakini papara ya kutaka kuwaonyesha wanaofikiri hawawezi wamekosea, inachangia kwa kiasi kikubwa yeye kushindwa kufanya vema kama anavyotaka.

CHIRWA ANAAMINI ATAENDELEA KUFUNGA, IKISHINDA ITAKUWA HIVI...

Obey Chirwa amesema yeye ni mfungaji, anataka kuendelea kufunga mabao kwa ajili ya kikosi chake cha Yanga. Chirwa raia wa Zambia ana mabao matano, anasema anataka zaidi ili kujiongezea morali. Lakini kama itashindikana kabisa, anachotaka ni kuisaidia timu yake kupata ushindi. “Nikifunga, timu inapata ushindi. Nisipofunga basi ntajitahidi kuisaidia timu ili ipate ushindi pia. “Kikubwa kwa pamoja tunataka timu ishinde bila kujali anafunga nani,” alisema Chirwa ambaye ni mtaratibu. Chirwa amejiunga na Yanga akitokea FC Platnums ya Zimbabwe na alianza kwa ugumu kwa kuwa hakuwa amefunga. Katibu wa Baraza la Wazee wa Yanga, Ibrahim Akilimali aliwahi kusema hana lolote. Lakini mwisho alipoona ameanza kupachika mabao akasema; “Chirwa ni jembe wewe, nilikuwa namtia upepo tu.”

MSIYEMTAKA KAREJEA, BALOTELLI APIGA BAO BAADA YA KUMALIZA ADHABU YA KADI NYEKUNDU, NICE YABAKI KILELENI UFARANSA

Amecheza mechi: 5 Kafunga mabao: 6 Usahihi wa mashutu: 86 % Nafasi alizotengeneza: 1 Uhakika wa pass: 75 % Msaada wa ushindi: 42 % Kadi za njano: 2 Kadi za nyekundu: 1

COSTA, HAZARD WACHEKA NA NYAVU CHELSEA IKIITULIZA SOUTHAMPTON MBILI MTUNGI

SOUTHAMPTON (4-3-3-): Forster 6.5; Martina 5, Fonte 6, Van Dijk 6.5, Bertrand 6 (McQueen 78); Romeu 6, Clasie 5 (Boufal 61), Davis 6; Redmond 6, Tadic 5 (Hojbjerg 78), Austin 5 SUBS NOT USED: Taylor, Yoshida, Ward-Prowse, Olomola MANAGER: Claude Puel 6 CHELSEA (3-4-3): Courtois 6; Azpilicueta 7, Luiz 7, Cahill 6.5; Moses 7.5 (Ivanovic 87), Kante 7 Matic 7.5, Alonso 6; Pedro 6.5 (Willian 78), Costa 8.5 (Batshuayi 88), Hazard 8 SUBS NOT USED: Begovic, Oscar, Terry, Chalobah GOALS: Hazard 6, Costa 55 MANAGER: Antonio Conte 7 REFEREE: Mike Jones 6 ATTENDANCE: 31,827 MAN OF THE MATCH: Diego Costa

Full time: Southampton 0-2 Chelsea Brilliant at the back and great in attack. The three points are ours!

LIVE KUTOKA UWANJA WA UHURU; YANGA 3 VS 0 MBAO FC (FULL TIME)

MPIRA UMEKWISHA -Mbao wanapata kona baada ya Bossou kuutoa mpira, inachongwa lakini Yanga wanaokoa DAKIKA 2 ZA NYONGEZA KADI Dk 88, Kipa Dida analambwa kadi ya njano kwa kuchelewesha mpira kwa makusudi Dk 87 sasa, Mbao wanaonekana kuamka na kutaka kupata bao angalau moja, lakini bado Yanga wako vizuri zaidi Dk 84 sasa, Yanga wanaonekana kuupoza mchezo huku Mbao kama wamekata tamaa ingawa mara kadhaa wanajitahidi kushambulia Dk 80 Ndikumana anapiga mkwaju wa adhabu hapa, lakini Dida anadaka kwa ulaini kabisa Dk 78 sasa, kwa hali ilivyo, Mbao wanaonekana kupoteana kabisa, Yanga wanapiga pasi wanavyotaka. Lazima Mbao FC waimarishe uchezaji wao kwenye kiungo, la sivyo Yanga wanaweza kushindilia bao la nne GOOOOOOOOO Dk 75, Tambwe anaifungia Yanga bao safi kabisa akiunganisha pasi safi ya Simon Msuva DK 74, Donald Ngoma anaruka na kupiga kichwa mpira wa kurusha wa Twite, lakini safari hii kipa yuko makini SUB Dk 71, Yanga wanamtoa Chirwa na nafasi yake inachukuliwa na Donald Ngoma KADI Dk 70 Ndikumana analambwa kadi ya njano kwa kumkwatua Haji Mwinyi SUB Dk 64, Yanga wanamtoa Hassan Kessy na nafasi yake inachukulwia na Thabani Kamusoko, maana yake Mbuyu Twite anakwenda pembeni kulia Dk 62, Tambwe anaachia kombora hapa linagonga mwamba na kutoka nje, ilikuwa ni al manusura SUB Dk 56, Juma Mahadhi anaingia kuchukua nafasi ya Kaseke GOOOOOOOOOO Dk 55, mpira wa kurusha wa Twite unakwenda moja kwa moja kwa moja wavuni kipa kuupangulia ndani SUB Dk 54 Venance Ludovic anaingia Damas Msiba kwa upande wa Mbao FC Dk 50, Yanga wanazidi kusukuma mashambulizi, Niyonzima anaangushwa hapa, anatibiwa GOOOOOOOOO Dk 49, Bossou anafunga bao lakini mpira unagusa mkono wake kabla ya kuingia wavuni. Ilikuwa ni baada ya kuunganisha krosi ya Niyonzima aliyepiga mpira wa adhabu Dk 46, Yanga wanaanza kwa kasi wakishambulia zaidi na wanaonekana wanataka bao la mapema MAPUMZIKO DAKIKA 2 ZA NYONGEZA Dk 44, Tambwe anapokea pasi nzuri ya Niyonzima na kupiga vizuri lakini mpira unatoka kiduchu kabisa SUB Dk 42, Salum Sued anakwenda nje kwa upande wa Mbao FC, nafasi yake inachukuliwa na Maganga Dk 37, Bado hakuna hata shambulizi kubwa. Inaonekana wazi Yanga wanahitaji mtu wa kulazimisha kama Ngoma vile. Chirwa na Tambwe wanaonekana 'kutoiva' pamoja Dk 30, bado inaonekana hakuna shambulizi kali zaid ya kona. Dk 24, Mbao wanapata kona baada ya Bossou kulazimika kutoa nje mpira, inachongwa lakini Dida anadaka vizuri kabisa Dk 18, Yanga inapata kona ya kwanza baada ya beki Mbao kumuwahi Msuva na kuutoa. Inachongwa lakini haina manufaa Dk 14, hakuna shambulizi kali kwa upande wowote, inaonekana kila upande bado haujajipanga katika umaliziaji Dk 8, Chirwa anapiga shuti kimo cha nyoka lakini linatoka sentimeta chache kabisa nje ya lango la Mbao Dk 6, krosi safi ya Kaseke, Msuva anaunganisha vizuri kabisa lakini anashindwa kulenga lango. Yanga imetumia takribani dakika nne ikigongena vizuri kabisa Dk 1 mpira unaanza taratibuuu kila upande unaonekana ukiwa makini kwa kutaka kufunga na kuepuka kufungwa

Mayanja ameitaja sababu ya kumtoa Mavugo katikati ya kipindi cha kwanza Mwadui vs Simba

Inawezekana kabisa kuna watu walishangazwa kumshuhudia mshambuliaji wa Simba Laudit Mavugo akipumzishwa katikati ya kipindi cha kwanza na nafasi yake kuchukuliwa na Ame Ali ‘Zungu’ katika mechi ya Mwadui 0-3 Simba, mara baada ya game hiyo kumalizika nikamtafuta kocha msaidizi wa Simba Jackson Mayanja kutoa sababu ya benchi la ufundi kumpumzisha Mavugo. Mayanja amesema Simba haitegemei mchezaji mmoja, kikosi kimesimama vizuri ndiyo maana kwenye mchezo wao dhidi ya Mwadui, Ibrahim Mohamed amefunga magoli mawili. Kuhusu kumpumzisha Mavugo, Mayanja amesema: “Kama mchezaji hafanyi vizuri unamtoa anaingia mwingine kuchukua nafasi ili abadili mchezo,” alisema Mayanja muda mchache baada ya kumalizika kwa mechi ya Mwadui vs Simba. Mechi iliyopita ya Simba dhiti ya Toto Africans, Mavugo alianzia benchi lakini aliingia kipindi cha pili baada ya Fredrick Blagnon kuumia na kushindwa kuendelea na mchezo. Mavugo alifunga goli moja kwenye ushindi wa Simba 3-0 Toto Africans.

OMOG AFURAHIA USHINDI WA SIMBA SHINYANGA LAKINI ATAKA MABAO ZAIDI TENA

Simba imezidi kujikita kileleni baada ya kuitwanga MWadui FC kwa mabao 3-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, jana. Pamoja na hivyo, Kocha wa Simba, Joseph Omog amesisitiza kuwa lazima kikosi chake kihakikishe kinashinda mabao zaidi ingawa suala la viwanja vya mikoani ni tatizo. "Viwanja vya mikoani ni tatizo kwa kweli, unaona ni kiwango duni na inakuwa ni tatizo kwa wachezaji na afya yao. "Lakini bado tunatakiwa kushinda mabao zaidi hasa kwa kuwa nafasi tunazipata, lazima kuzitumia," alisema. "Soka ni mchezo wenye makosa, mnatakiwa kuendelea kujifunza kila siku. Tunaendelea kurekebisha jambo kila baada ya mechi moja." Simba ilishinda tatu, mabao mawili yakifungwa na Mohammed Ibrahim na moja likifungwa na Shiza Kichuya. Lakini Simba ilipoteza zaidi ya nafasi mbili safi kabisa za kufunga kupitia kwa Laudit Mavugo na Muzamiru Yassin.