Jumapili, 25 Septemba 2016

MATOKEO VPL KUTOKA KAMBARAGE SHINYANGA: STAND UNITED 1 VS YANGA 0 (FULL TIME)

MPIRA UMEKWISHAAA -Stand wanachofanya sasa ni mambo mawili, ni kupoteza muda na kubutua mpira -Tambwe anapiga shuti kali hapa, lakini unakwenda mikononi mwa kipa wa Stand DAKIKA 5 ZA NYONGEZA DK 90, Twite anarusha mpira, lakini beki ya Stand wanaokoa na kuwa kona. Inapigwa lakini, goal kick Dk 87, beki Mlilo wa Stand akiwa chini pale na mpira umesimama tena SUB Dk 86, Yanga wanamtoa Haji Mwinyi na nafasi yake inachukuliwa na Haruna Niyonzima SUB Dk 85, Stand wanamtoa Kingwande na nafasi yake inachukuliwa na Abaslim Chidiebele Dk 82, Kingwande anapoteza nafasi nzuri kabisa akiwa uso kwa uso na kipa Barthez, Dante anaokoa vizuri kabisa Dk 79, Job anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira wa Juba Abdul, inakuwa kona. Inachongwa lakini Stand wanaokoa hapa SUB Dk 77, Ngoma anakwenda nje upande wa Yanga na nafasi yake inachukuliwa na Obey Chirwa Dk 76 sasa, bado mpira haujatulia, Yanga wanajaribu kushambulia kwa kasi lakini Stand wao wanaonekana kubutua zaidi KADI Dk 74 Ngoma analambwa kadi ya njano kwa kumtwanga teke Adam Kingwamnde KADI Dk 72, Frank Khamis wa Stand analambwa kadi ya njano kwa kubutua mpira baada ya kipenga SUB Dk 70 Kipa Mhonge wa Stand analambwa kadi ya njano kwa kupoteza muda Dk 67, Msuva anapiga shuti kali la mpira wa adhabu lakini linapaaa juuu Dk 65 Krosi ya Bossou, Tambwe anapiga kichwa safi lakini Muhonge, kipa wa Stand kutoka Uganda, anadaka vizuri kabisa huku akiweka mbwebwe Dk 64 sasa, Yanga wanafanya mashambulizi mfululizo kuhakikisha wanasawazisha SUB Dk 62, Yanga wanamtoa Kaseke na nafasi yake inachukuliwa na Juma Mahadhi, mashabiki wa Stand wanaendelea kuimba kwa shangwe GOOOOO Dk 60, Pastory Athanas anaifungia Stand bao safi kwa shuti kali baada ya beki Haji Mwinyi kutaka kuupata rangi mpira 56, mechi inaendelea baada ya Job kutolewa na wachezaji wa Yanga na Stand wanagongana tena, wako chini pale ni Tambwe na Adeyum Dk 51, Job anagongana na kipa wake, Muhonge pamoja na ngoma, mpira unasimama, anatibiwa kwa takribani dakika mbili Dk 47, Yanga wanaanza kushambuliakwa kasi kubwa, lakini Stand wanaonekana kuwa makini MAPUMZIKO -Krosi safi ya Msuva, lakini Kaseke anaonekana alifumba macho, mpira wa kichwa aliopiga unakuwa goal kickDAKIKA TATU ZA NYONGEZA Dk 45, Msuva anafanyiwa madhambi na Ibrahim Job, yuko chini anatibiwa na mpira umesimama Dk 43, Stand wanagongeana vizuri lakini Dante anakuwa makini na kuondosha hatari Dk 40, hakuna timu yenye uhakika wa bao hadi sasa na basi zinaonekana kupigwa katikati ya uwanja zaidi Dk 37, kipa wa Stand United anaudaka kwa ustadi mkubwa mpira wa faulo wa Thabani Kamusoko, lakini analala chini kuwa ameumia KADI Dk 36, nahodha wa Stand, Jacob Masawe analambwa kadi ya njano kwa kuzuia mpira usichezwe Dk 35, Yanga wanapoteza nafasi nzuri baada ya Ngoma kuukosa mpira wa kona iliyochongwa na Msuva SUB Dk 33 Stand wanafanya mabadiliko ya kwanza kwa kumuingiza Frank Khamis kuchukua nafasi ya Jeremia Khatura Dk 30, ni nusu saa sasa, Stand wanaonekana kushambulia zaidi lango la Yanga. Dk 29, Stand United wanaonekana kutulia na kuwasumbua sana Yanga. MAshambulizi yao ni makali zaidi na Yanga wanapaswa kuwa makini la sivyo watajilaumu DK 28, Kelvin Sabato anamtoka Dante na kuingia vizuri, anapiga shuti kali lakini linaokolewa na kipa Mustapha na kuwa kona. Inachongwa, haina manufaa Dk 24, Msuva anatoa pasi safi kabisa kwa Ngoma, lakini anaugusa mpira kidogo sana unaangukia mikononi mwa kipa Dk 23, krosi nzuri ya Pastory Athanas lakini barthez anafanya kaz ya ziada kuokoa, kona. Inachongwa na Yanga wanaokoa Dk 20, Ngoma anapambana na mabeki wawili wa Stand na kunpa pasi Tambwe lakini anapiga shuti kuuubwaa Dk 19, Yanga wanagongeana vizuri, mpira unamfikia Kamusoko, anapiga shuti lakini kipa anadaka vizuri Dk 16, Yanga wanaingia vizuri, Msuva anajaribu kuuwahi mpira, hata hivyo anadhibitiwa Dk 14, Kimngwande anawatoka mabeki wawili wa Yanga akiwemo Bossou, lakini hata hivyo kasi yake inakuwa ndogo Dk 12, nafasi nzuri kabisa kwa Stand United lakini Adam Kingwande anapoteza akiwa amebaki yeye na Mustapha DK 8, mpira unakwenda taratibu sana na hakuna timu inayoonyesha kupatia kupata bao. Dk 5, beki Adeyum Saleh wa Stand anajigonga kwa Msuva na kuanguka, anatibiwa hapa na baadaye anarejea. Kidogo alianguka vibaya Dk 3, hadi sasa hakuna shambulizi kali upande wowote, Yanga wamepata kona lakini bado haikuwa na madhara yoyote kwa Stand Dk 1, Yanga ndiyo wanakuwa wa kwanza kufika katika lango la Stand United, lakini inaonekana wachezaji wa Yanga, waliishaotea.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni