Kumekuwa na tafrani kubwa katika vipindi kadhaa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, hasa usiku huu.
Mashabiki na wanachama wa Yanga na Simba, wameendelea kuulinda uwanja huo, kila mmoja akiwa na hofu na mwenzake.
Umakini umeongezeka huku kila upande ukiwa na hofu ya mwingine ‘kummaliza’ mwenzake.
Pamoja na kulindana, makundi yote yamekuwa yakionekana kutoamini jingine na mara kadhaa wamekuwa wakirushiana maneno.
Jana, baadhi ya mashabiki na wanachama wa Yanga, walimpa wakati mgumu mmoja wa wanachama wa Simba aitwaye Makoye wakimtuhumu kuwazidi ujanja na “kufanya mambo yake”.
Hali ambayo imesababisha wengi kuwa makini na wakali huku upande wa Simba nao wakijibu mapigo.
Suala la ushirikina, limekuwa tatizo kubwa. Pamoja na maandalizi ya vikosi, suala la kutoaminiana na hofu ya kufanyiana ushirikina, imekuwa kubwa sana kila inapofika mechi ya Yanga na SImba.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni